TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 18 Januari 2016

JAHAZI KOROMBWE WATOA KAULI JUU YA WAO KUPIGWA MARUFUKU KUPIGA NYIMBO ZA JAHAZI MODERN TAARAB.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                Mkurugenzi wa korombwe modern taarab au ukipenda "jahazi korombwe" Babu chollo leo amezungumza na mtandao huu juu ya barua waliyoletewa na uongozi wa bendi ya jahazi modern taarab kuhusu kusitisha mara moja wao kupiga wimbo wowote wa bendi ya jahazi modern taarab katika show zao wanazozifanya.

BABU CHOLLO-MKURUGENZI WA JAHAZI KOROMBWE MODERN TAARAB.
              Akizungumza kwa kujiamini Babu chollo alisema kwamba anashangazwa na uongozi wa jahazi kuwaletea barua wao eti waache mara moja kupiga wimbo wowote wa jahazi modern taarab huku mzee akisahau kwamba hata yeye wakati anaanzisha bendi yake hiyo alikuwa anapiga copy ya nyimbo za zanzibar star's na east african melody,.. mzee amewahi mpaka kurekodi upya wimbo wa mazoea yana tabu huku akijua wazi kuwa si wake kwani ile sio copy?.

             Labda mimi nimkumbushe mzee kwamba amewahi kuja katika moja ya maonyesho yetu yeye akiwa na mkewe leyla rashid na baada ya kupenda kile tukifanyacho alinyanyuka na kuja mbele kutunza elfu kumi, yote hii inaonyesha wazi kwamba alifurahia kile tukifanyacho!, sasa labda kama ana chuki zake binafsi aseme wazi tu!, kingine iweje barua iletwe katika bendi yetu tu huku kukiwa na bendi nyingi ambazo zinapiga nyimbo za jahazi? alihoji. mimi napenda kuchukuwa nafasi hii kusema kwamba sina tatizo na mzee yusuph wala kiongozi yeyote wa jahazi, barua yao tumeifanyia kazi na hatupigi tena nyimbo za jahazi modern taarab isipokuwa tutakuwa tukipiga nyimbo zetu wenyewe tu pamoja na nyimbo za zanzibar star's na east afican melody kama ikibidi. Ndugu mwandishi hakuna hata bendi moja ya taarab tanzania hii ambayo ilianzishwa na kutokupiga nyimbo za copy...si kweli nakataa!, na ndio maana watu wa taarab hatuendelei sababu ya chuki zisizo na kichwa wala miguu.

           Mtandao huu ulipata bahati ya kuiona hiyo barua ya jahazi modern taarab kwenda korombwe modern taarab na iliandikwa kama ifuatavyo:-

                                                                                          JAHAZI MODERN TAARAB
                                                                                                P.O. BOX 110191 Dar es salaam Tanzania
                                                                                                 Tel NO. 0655 888 889/ 0767 002 315
                                                                                                                         0689 109 022

                                                                                                                    06/01/2016

                                                       KWA YEYOTE ANAEHUSIKA.

                                                    YAH:- KUZUIA KUPIGWA NYIMBO ZETU

                               Rejea kichwa habari hapo juu.

               Jahazi modern taarab imezuia kupigwa nyimbo zake katika rusha roho/ bendi zote za taarab, mpaka kwa makubaliano maalum kutoka kwa uongozi wa jahazi modern taarab.

                                                              Wako
                                                             ........................
                                                         MZEE YUSUPH
                                            MUKUGENZI MKUU-JAHAZI MODERN TAARAB.

NAKALA:-
1.BASATA
2.Afisa utamaduni
3.Polisi
4.Bendi zote za taarab
5.Wapiga rusharoho.

                         Baada kuisoma barua hii dawati la habari la ubuyu wa taarab liliamua kumtafuta mkurugenzi mkuu wa jahazi modern taarab mzee yusuph na kutaka ufafanuzi juu ya kipengere kinachosema "mpaka kwa makubaliano kutoka kwa uongozi" ni yapi haya makubaliano? je wapo tayari kukaa chini na bendi zinazopiga copy zao ili wayazungumze yaishe?.na mzee alijibu kama ifuatavyo:- kwanza mimi sikuwaambia viongozi wangu waandike kitu kama hicho...makubaliano...makubaliano gani tena? mimi nimekataza kupigwa nyimbo za bendi yangu na sina mjadala na mtu! kama wao viongozi wa jahazi wameandika hivyo si sawa kabisa, na nawasiliana nao muda mchache ujao ili waondoe kipengele hicho kama kweli wamekiandika maana leo barua zingine zinasambazwa pia katika bendi ambazo zinapiga nyimbo zetu bila idhini.

.
MZEE YUSUPH-MKURUGENZI WA JAHAZI MODERN TAARAB.
                        Ikumbukwe wiki mbili zilizopita mtandao huu uliandika habari zilizokuwa zikimuhusu mzee yusuph kupiga marufuku kwa bendi yoyote kupiga nyimbo za bendi yake ya jahazi modern taarab katika show zao.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni