Jokha kassim mamaa wa domo la udaku wimbo ambao unaendelea kufanya vizuri kupitia media mbalimbali hapa nchini tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi hii, amezungumza na mtandao huu kwa njia ya simu na kufunguka juu ya mapromota ambao wamekuwa wakichukua show huko mikoani na kuwadhurumu.
Aliyasema haya baada ya kutupiwa swali kuhusu pesa ambazo jokha kassim ilisemekana ametapeli huko kilosa baada ya kupatiwa advance ya show na yeye kutotokea kabisa jambo lililopelekea promota huyo kumchafua sana jokha kassim mitandaoni akilalama kwa kile alichofanyiwa na msanii huyo. Akijibu tuhuma hizo jokha kassim alisema kwamba ni kweli nilitumiwa pesa na huyo kaka lakini nami nilipatwa na tatizo la ghafla mwanangu alirudishwa toka shuleni anaposoma maana yupo bording na kufikishwa moja kwa moja muhimbili maana alikuwa ana homa kali sana na alilazwa pale, sasa mimi kama mzazi naanzaje kusafiri katika show kilosa katika mazingira kama hayo? alihoji jokha kassim.
Ila baadae nilizungumza na yule promota na kumuahidi kumlipa pesa yake ambayo alinitumia, ila hawa mapromota ni watu wabaya sana kwani mimi nimeshatapeliwa sana huko mikoani, mtu anakuita katika show ukifika mnafanya show lakini inapokwenda kinyume na matarajio yake anakukimbia na kukuacha solemba! mimi yameshanitokea sana huko mikoani lakini nanyamaza tu ila naahidi ipo siku nitawaanika wale wote ambao walinitapeli na kuniingiza mjini, wasinione mimi mjinga kunyamaza kimya!, siku hizi nimejifunza kutokana na makosa, promota anaponihitaji mimi basi anatakiwa kunilipa asilimia 80% ya tulichopatana alafu baadae kilichobakia tutalipana nitakapofika huko maana nimechoka kutapeliwa kusema kweli alimaliza kwa kusema jokha kassim.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni