Muimbaji chipukizi an amekuja kwa kasi kubwa mwajuma kidoti ambae kwa sasa yupo katika bendi ya majaz modern taarab ameshangazwa na taarifa zilizozagaa kuwa yeye kwa sasa ni mali ya jahazi modern taarab.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mwajuma alisema kwamba taarifa za yeye kujiunga na jahazi modern taarab sio kitu kibaya isipokuwa hajafikia makubaliano rasmi kimaslahi na viongozi wa bendi hiyo. Ni kweli nilipigiwa simu na kiongozi mmoja wa bendi hiyo akinifahamisha kuwa natakiwa katika bendi hiyo kuongezea nguvu lakini hatujaelewana chochote kile kwahiyo mimi mpaka sasa ni msanii halali kabisa wa majaz modern taarab.
Mtandao huu uliwatafuta viongozi wa bendi ya jahazi lakini taarifa zilizopatikana walikuwa katika kikao kikubwa na kampuni moja ambayo inataka kupeleka bendi hiyo nchini Rwanda katika tamasha maalum la nyimbo za kimwambao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni