TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 21 Desemba 2014

FADHILA MNOGA, MDOGO WA HADIJA MNOGA KIMOBITEL ANAESUMBUA G5 MODERN TAARAB KWA SASA.

NA KAIS MUSSA KAIS

         Kuna msemo wa kiswahili usemao 'Maji hufuata mkondo", Fadhila Mnoga ni muimbaji wa bendi ya G5 Modern Taarab yenye makazi yake mtoni kwa Azizi Ally jijini Dar, Huyu ni mdogo wa Khadija Mnoga kimobitel ambae anaimba miondoko ya Dansi kwa sasa. Unapotembelea pale Flamingo Night Club ukamuona Fadhila akiwa steji na bendi ya G5 utakubaliana na mimi kwamba huyu msichana anaweza sana na ni hazina ya baadae katika muziki huu wa taarab nchini Tanzania.

FADHILA MNOGA AKIWA KATIKA POZI.
          Fadhila Mnoga amezunguka bendi nyingi ndogondogo kabla mwaka jana hajajiunga na bendi ya Dar Modern Taarab, lakini kwa bahati mbaya hakukaa sana kwani alikuwemo katika wale wasanii 13 ambao walifukuzwa katika bendi hiyo baada ya kurudi safari na Dar Modern toka mikoani, iliniuma sana kufukuzwa bendi kwa kosa nisilotenda lakini mungu alikuwa na mipango yake kwangu, na kwa sasa nipo hapa G5 Modern Taarab maisha yanaenda kama kawa kama dawa!.

      Taarab ni muziki niupendao sana na nafanya kwa mapenzi makubwa mnoo!, hapa G5 Modern Taarab nipo na ndugu yangu anaitwa Sharifa Mnoga nae ni muimbaji mzuri sana, sisi katika familia yetu wengi ni waimbaji ukimtoa Dada Hadija ambae tayari anafahamika lakini tupo na sisi tunafuata nyayo zake pia.


FADHILA MNOGA AKIWA NA DADA YAKE HADIJA MNOGA "KIMOBITEL".
         Fadhila Mnoga bado hajarekodi wimbo wowote G5 ila yupo mbioni kupewa wimbo mpya ambao ndio atatoka nao na watu kuelewa uwezo wake, kwa sasa anaimba sana nyimbo za G5 ikiwemo wimbo uliorekodiwa na dada yake Hadija Mnoga uitwao "Naepuka Mifarakano". njoo umuone akiimba ndani ya bendi hiyo pale Flamingo Night Club magomeni mwembechai Dar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni