TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 24 Desemba 2014

JE UNAJUA MZEE YUSUPH ALIANZA VIPI MUZIKI WA TAARAB?...BASI USIPITWE MSOME HAPA!.

NA KAIS MUSSA KAIS

          Katika muziki wa taarab, Mzee yusuph ni mtu alieleta changamoto kubwa sana mpaka sasa, lakini je unajua alianzaje kuimba muziki huu?, ungana nami katika mahojiano haya:-

SWALI: Sasa turudi upande wa historia yako, labda tueleze ulizaliwa lini ukakulia wapi, maisha yako kwa ujumla.

JIBU: Nimezaliwa miaka 1977 na nimezaliwa Zanzibar. Nimelelewa kulekule nimekulia kulekule na kazi zangu nilianza kule kule za usanii, na nimemaliza darasa la 10 Zanzibar katika shule ya Haile Selasie.
Sikuwa nataka tena kuendelea na shule sababu niliona hali ngumu, si unajua maisha? nkaona hata! Hii ndio itanipeleka hii, sa niache huku. Niache moja nikamate moja.

Kwa hiyo niliacha shule, sikuendelea darasa la kumi na moja. Nikaanza mziki. Nilikuwa nafanya mziki nafanya maigizo, niko na shule, sa ilifika pahali sa nikachukuliwa na bendi ya melody.
Sa nkaona kidogo hapa kuna maslahi japo nilikuwa ‘napigwa buku kwa siku’ (nalipwa shilingi elfu moja kwa siku), lakini nilikuwa nashukuru sababu nilikuwa siipati ile buku,
MFALME MZEE YUSUPH PICHANI.
SWALI: Sasa umeingia katika mziki wa taarabu. Ni muziki ambao kwa kweli unapendwa. Wengi wakisema mziki wa mwambao, wengine hivi, alimradi kila mtu na lugha yake anavyouita mziki huu. Ulipata ushawishi gani mpaka ukaingia katika ulimwengu huu wa mziki wa taarabu?.

JIBU: Kwa kweli labda unajua kwa nilipokuwepo taarabu ndio ilikuwa inapendwa na nilikuwa na uwezo wa kuimba taarabu si vingine.
Na sikutegemea kama mtakuwa labda nami naweza kutunga nini mm’kh! Nilikuwa nahisi naweza kuimba. Sababu hata tulikuwa tunakaa nyumbani, tulikuwa tunamsikiliza mother (mama) anaimba, anaimba taarabu, tunakaa naye anatufahamisha hii inaimbwa hivi, hii ndio hivi, hii ndio hivi.
Sa ikafika mahali yani ile muziki ukawa unanijaa. Unanijaa sana kiasi ikafika mahala kwenye mazoezi ya mpira nawaambia wenzangu mimi ntakuwa naimba taarabu.
Basi kwa sababu nilikuwa napenda, halafu ni kwamba uwezo nilikuwa nao. Pale ndo nilipokuwa na ilo nivutia, lakini sio kuwa nilifikiria labda kumuona mtu mmmhkh! Sababu nilikuwa naweza.
Halafu mama yangu mzazi alikuwa mwimbaji wa taarabu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni