TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 18 Desemba 2014

KIFO CHA AISHA MADINDA NI UTATA MTUPU!.

NA KAIS MUSSA KAIS

 
Mwanamuziki na Mnenguaji wa Bendi  ya African Stars “Twanga Pepeta”, Aisha Madinda amefariki dunia  Jana.
 AISHA MADINDA ENZI ZA UHAI WAKE

Taarifa zilizotufikia zimesema mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam huku chanzo cha kifo chake kikiwa cha kutatanisha
Mmiliki wa Bendi hiyo Asha Baraka amekaririwa akisema alipewa taarifa na daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.
Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea,” alisema Asha Baraka
Historia ya Aisha Madinda
Aisha Madinda ambaye jina lake halisi ni Aisha Mbegu alizaliwa mwaka 1980 katika  Hospitali ya Ocean Road jijini Dar na alipata umaarufu mkuwa kwa uhodari wake wakucheza muziki alipokuwa kwenye  Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Vile vile Aisha aliwahi kuingia kwenye tasnia hii ya filamu na kuweza kuigiza filamu akiwana watu kama aliyekuwa mwimbaji TX Moshi William (Marehemu)  pamoja na mcheza soka Boniphace Pawasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni