NA KAIS MUSSA KAIS
Mnenguaji Aisha Madinda aliyefariki jana asubuhi, atazikwa kesho mchana badala ya leo kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Mtoto
wa kwanza wa marehemu Aisha Madinda, aitwae Feisal amemwambia mwandishi wetu kuwa polisi wamesema ni
lazima mwili wa mama yake ufanyiwe upasuaji ili kujua
chanzo cha kifo chake.
![]() |
AISHA MADINDA ENZI ZA UHAI WAKE. |
Awali
ndugu wa marehemu walisema hawahitaji mwili wa mpendwa wao Aisha Madinda ufanyiwe upasuaji,
lakini baada ya polisi kutembelea eneo la tukio la kifo chake huko
Mabibo, wamesema ni lazima upasuaji ufanyike.
Feisal amesema upasuaji unatarajiwa kufanyika leo mchana hali inayowalazimisha kubadili ratiba ya mazishi.
Aisha Madinda sasa atazikwa kesho mchana baada ya sala ya Ijumaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni