Bendi yako uipendayo ya 5 Stars Modern Taarab, siku ya ijumaa tarehe 19/12/2014 inatarajia kufanya uzinduzi wa Albam yake mpya iitwayo "Kichambo kinakuhusu", albam hiyo ambayo imekuwa ni gumzo kwa sasa hapa mjini itazinduliwa katika ukumbi wa Travetine magomeni jijini Dar kuanzia saa tatu kamili za usiku.

Bendi ambazo zitasindikiza uzinduzi huo sambamba na wasanii mmoja mmoja ni wakaliwao modern taradance na mkombozi Thabit Abdul, Ogopa Kopa chini ya malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa, Abdul Misambano, Ashura Machupa, Jokha Kasim, kibao kata na Bi Mwanahawa Ally. Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi ya 5 stars modern taarab Ally J alisema vijana wake wamejipanga vyema na kwa hivi sasa wapo kambini wakijifua zaidi ili kufanya maajabu siku ya tukio.
Ikumbukwe kwamba bendi ya 5 stars modern taarab imeongeza waimbaji wengine wapya ambao ni Salha Abdallah au ukipenda muite Salha wa Hammer Q, Pia wamemchukuwa Mape Kibwana muimbaji ambae alikuwa Dar Modern hapo nyuma, vile vile yupo Mariam B.S.S, Mussa kijoti na wengineo. kiingilio katika uzinduzi huo ni shilingi elfu 5 kama ukikata tiketi mapema na shilingi elfu 7 kama utakata mlangoni siku ya onyesho usikose!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni