TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 15 Desemba 2014

TAARIFA MUHIMU KWA WATANGAZAJI WOTE WA VIPINDI VYA TAARAB NA WADAU WA BLOG HII BORA!.

NA KAIS MUSSA KAIS

            Mtandao wa ubuyuwataarabutz,blogspot.com Kwa furaha na bashasha kubwa unapenda kuwafahamisha watangazaji wote wa vipindi vya taarab katika redio na hata televisheni kwamba wanaweza kutuma picha zao pamoja na maelezo ya vipindi vyao, nasi tutaweka katika blog hii ili kuwatangazia bure kwa muda wa wiki moja baada ya picha kutufikia..

HUYU NI MTANGAZAJI WA BOMBA FM MBEYA, ANAITWA AMANI MBILO "KADADAA AU MJUKUU WA MPIGA MITI", JE WEWE UNASUBIRI NINI?.
         Tumeamua kufanya hivi baada ya kutambua umuhimu wenu kwetu katika kusoma habari ambazo zimekuwa zikiandikwa humu kupitia vipindi mnavyorusha, kikubwa msisahau kuitaja blog hii ya ubuyuwataarabutz.blogspot.com kwani ni imani yetu kubwa kwamba ninyi na sisi tumekuwa tukitegemeana katika kuwapasha habari wapenzi wa muziki wa taarab duniani kote. Hata wale wenye redio za ONLINE nchi za nje lakini wanafanya taarab wanaweza kututumia picha nasi tukaziweka katika blog hii, kumbuka kuwa baada ya picha yako kukaa kwenye blog hii kwa wiki moja, basi itatolewa ili kupisha na wengine nao kupata nafasi.

       Changamkia ofa hii kwani kwa sasa blog hii inasomwa na mataifa mbalimbali duniani kote so! itakuwa ni faida kwako na kwa kituo unachofanyia kazi pia. Unachotakiwa kufanya ni kunitumia "inbox' maelezo yako sambamba na picha kwenye acount yangu ya facebook ambayo ni kais mussa kais  nami bila hiyana nitaiweka na utajiona bila shaka. Kumbukeni kwamba hii ni blog yenu kwahiyo itumieni ili iwatangaze.

                                   AHSANTENI NYOTE!!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni