NA KAIS MUSSA KAIS
Shadya Othman au ukipenda muite "Shadya Shombeshombe" ni muimbaji wa Ogopa Kopa Classic bendi. Bendi ambayo inamilikiwa na malkia wa mipasho nchini tanzania Khadija Omary Kopa, pindi unapobahatika kuhudhulia onyesho lolote la bendi hii basi utakutana na binti huyu akiwa katika sura ya tabasamu, mng'avu na mwenye haiba ya kike haswa!.
 |
SHADYA SHOMBESHOMBE MUIMBAJI WA OGOPA KOPA!. |
Shadya kila unapozungumza nae hasiti kumshukuru sana Malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa kwamba ndio chachu haswa ya kufahamika kwake katika tasnia ya muziki huu wa taarab, nilipofika kwa mara ya kwanza hapa nikiwa na Hemedy Omary sikutegemea kama leo hii naweza kuwa ni miongoni mwa wanaounda kikosi hiki kilicho sheheni masuper star kama Anifa Maulidy "jike la chui", Zena Mohamedy, Hassan Ally, Jumanne Ulaya na wengineo wengi.
 |
SHADYA SHOMBESHOMBE NDANI YA POZI LA NGUVU!. |
Kwa sasa nimefanikiwa kurekodi wimbo wangu mpya ndani ya Ogopa Kopa uitwao " Aanzae havumi", wimbo huu ni utunzi wake Hemedy Omary ukipenda muite Sonara wa Maneno.Shukrani ziwaendee viongozi wangu kwa kuweza kuniamini na kunipa wimbo, nami nimeutendea haki kwa kuuimba vizuri sana. Nilipomuuliza amejipanga vipi katika kuhimili mikikimikiki ya wasanii wakubwa au kwa tafsiri ingine wale walio mtangulia? alijibu kwa kujiamini "Mimi sitishiki na majina najiamini sana na kipaji changu na kamwe sintorudi nyuma, hapa safari ndio imeanza, Ogopa Kopa ni kazi tu majungu hukoo kwao!.
Shadya anaonekana ni mwanamke anaejiamini sana na kazi yake, sisi mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Tunamtakia mafanikio katika safari yake ya muziki na awe anasikiliza sana ushauri wa malkia katika kuweza kufikia malengo yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni