Bendi ya Wakaliwao Modern Taradance ni miongoni mwa bendi ambazo ziliteuliwa kushiriki Tamasha la Mitikisiko ya Pwani mwaka huu 2014 katika ukumbi wa Dar Live mbagala jijini. Lakini katika taarifa iliyoandikwa na mtandao huu leo mchana ilizungumza juu ya kutokupanda steji kwa bendi hiyo kutokana na sababu zisizofahamika, na tuliwaahidi wasomaji wa mtandao ubuyuwataarabutz.blogspot.com kwamba tutafuatilia kwa karibu mpaka tujue nini sababu iliyopelekea bendi hii isipande steji.
![]() |
THABIT ABDUL "MKOMBOZI". |
Nimeumizwa sana na hali hii ila sikuwa na jinsi waimbaji wangu walikuwa bado hawajafika, ikawalazimu Dar Modern wao wapande kuanza, nilijaribu kuwaomba waandaji kutupatia nafasi zaidi pindi walipokuwa wamefika waimbaji wangu lakini nilikataliwa kabisa nikiambiwa kwamba hapa tunakwenda kwa ratiba, muda wa Wakaliwao umeshapita kwahiyo mnaweza kurudi nyumbani.
Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba radhi wadau na wapenzi wote wa Wakaliwao kwa kile kilichotokea na nawaomba wasivunjike moyo kwa maneno yanayosemwa mitaani, Wakaliwao ni bendi yao na sisi tunawaahidi kuendelea kuwatengenezea mambo mazuri zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni