NA KAIS MUSSA KAIS
Baada ya siku mbili tu kupita tokea wimbo mpya wa Mariam B.s.s.kichambo kinakuhusu kuachiwa hewani, malalamiko yameanza kusikika toka kwa muimbaji wa Mashauzi Classic Abdul Malick akimtuhumu B.S.S. kwamba amemuimba yeye. Abdul Malick na Mariam B.s.s. hapo nyuma waliwahi kuwa wapenzi kabla ya kuachana baada ya mmoja kulewa umaarufu.
Baadhi ya maneno yaliyopo katika wimbo huo ambayo Abdul Malick analalamika kumlenga yeye ni kama "Bodi nyumba miguu ya nyongeza"..."Sura ngumu kama ganda la fenesi" na mengineyo ambayo yamesemwa humo, ikumbukwe kwamba Abdul Malick ni mlemavu wa miguu na ndio sababu kubwa ya kuumizwa na neno "Bodi nyumba miguu ya nyongeza". Unajua ndugu mwandishi mimi nimechoshwa na kashfa za huyu msichana, sasa safari hii nae ajiandae kuna kitu changu kinakuja katika album hii mpya ya mashauzi classic, ni utunzi wangu mimi mwenyewe wimbo utaitwa "Una laana za walimwengu".
Humo nimesema mengi sana zaidi ya sana, nimechoka kuonewa sababu ya ukilema wangu, kuimba najua, kutunga najua kila kitu naelewa ila nilikuwa nipo kimya tuu. Ila muda na wakati umefika wa mimi pia kuongea niliyokuwa nayo moyoni, naomba wadau wasubilie kitu kizuri kinakuja Very soon alimalizia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni