TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 19 Juni 2015

EL-HATIBU RAJABU:- UBORA WANGU UPO KWENYE TUNGO ZANGU, IPO SIKU ZAMU YANGU ITAFIKA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Mtunzi mahiri wa nyimbo nyingi za taarab hapa nchini El-Hatibu Rajabu ameibuka na kusema kwamba yeye hajali hata kama asipopata zawadi ya mtunzi bora wa muziki huo, ila ukweli utabakia pale pale kwamba yeye ndio ambae anaongoza kwa sasa kuzitungia nyimbo bendi karibia zote za taarab nchini.


EL-HATIBU RAJABU MTUNZI WA NYIMBO ZA TAARAB.

       Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu El-Hatibu alisema, ubora wangu umekuwa ukionekana kwa bendi nyingi za taarab, nimetungia bendi tofauti tofauti na nyimbo zimekuwa zikifanya vizuri tu!, mpaka sasa nimetungia bendi kama Jahazi modern taarab, Five stars modern taarab, Dar modern taarab, T motto modern taarab, Coast modern taarab na nyinginezo nyingi.


   Watu wamekuwa wakiniuliza najisikiaje kila mwaka katika tuzo za kilimanjaro music award's nakuwa sipati tuzo? lakini jibu langu ni kwamba zamu yangu haijafika ya kupata tuzo lakini naamini itafika tu!, siku zote mwenye subira huwa pamoja na mwenyezimungu. Nilipomuuliza anazizungumziaje tuzo za mwaka huu? alijibu kwamba nisingependa kuzungumza lolote katika hilo sababu tayari mashindano yameshaisha nisingependa kuanzisha mjadala mwingine tena!.


    Huyo ndie El-Hatibu Rajabu ambae mbali na utunzi wa mashairi lakini pia ana taaluma ya ualimu, mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com unapenda kumpongeza mtunzi huyu kwani amekuwa habahatishi kila anapotunga wimbo wowote, mpate katika Chongeni fenicha, Gubu la mawifi, Lauchungu halisahauliki, mwenyehila habebeki, Kichambo kinakuhusu, Domo la udaku na nyimbo nyingine nyingi sanaaaa!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni