Bendi ya king's modern taarab iliyo chini ya mkurugenzi wake Alhaji Kijoka "mzee wa kuzima taa" imekuwa haijulikani inafanya show zake wapi, baada ya mgawanyiko wa wasanii, na viongozi kuliko pelekea kuzaliwa kwa bendi ingine iitwayo Maja's Modern Taarab, iliyo chini ya mkurugenzi mwingine aitwae Hamisi Majaliwa
Dawati la Ubuyu wa taarabu kama kawaida yake lilipiga hodi nyumbani kwa mkurugenzi wa King's modern taarab Alhaji Kijoka huko maeneo ya mburahati jijini Dar, lengo ni kufahamu toka kwake yeye kama mkurugenzi ni kwanini wapo kimya sana tokea ulipotokea mpasuko wa kugawanyika kwa bendi mbili?. Unajua ndugu mwandishi bendi zipo nyingi sana sasa hivi, ushindani umekuwa mkubwa kwahiyo ni lazima nijipange kwanza nisikurupuke.
KUNDI ZIMA LA KING'S MODERN TAARAB |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni