TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 8 Novemba 2014

MSIBA! MSIBA!, AMIGO RASI BABAA NA SOPHY AFARIKI DUNIA!.

NA KAIS MUSSA KAIS

                    Wasanii, wapenzi na wadau wenzetu wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Tanzania wamefikwa na msiba mzito kwa kuondokewa na mwenzao au mwenzetu Amigo Rasi, Almaarufu Babaa na Sophy kama alivyokuwa akiitwa pale twanga pepeta, Taarifa za kifo chake zilianza kuzagaa kuanzia mida ya saa saba usiku na baadhi ya mitandao kuandika taarifa hizi za huzuni kwa wapenda muziki wote Tanzania.

AMIGO RASI ENZI ZA UHAI WAKE
            Unaweza kujiuliza inakuwaje Taarifa za Dansi zinaandikwa humu lakini kilichopo ni kwamba sisi sote ni familia moja ya muziki kwahiyo inapotokea zinapatikana taarifa za dharula kama hizi za msiba mzito kama huu basi hatuangalii ni wa kikundi gani, tasnia ipi wala umaarufu wa mtu! ni lazima ziandikwe ili watu waelewe kinachoendelea.


AMIGO RASI  KATIKATI AKIWA SAMBAMBA NA DOGO RAMA NA SALEHE KUPAZA, ENZI ZA UHAI WAKE!.
         Mpaka ubuyu wa taarabu unaingia mitamboni bado ilikuwa haijajulikana ni lini maziko yatafanyika na yatakuwa nyumbani kwake magomeni au lah!. Pindi zitakapopatikana taarifa za maziko yake basi tutawajuza humu humu shaka ondoa, Mwenyezimungu ailaze pema peponi roho ya marehemu Amigo Rasi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni