Kila msanii wa Taarabu, unapomuuliza nini malengo yako ya baadae katika muziki huu? basi atakuwa na maelezo mengi ya majibu ambayo yote yanalenga kupata mafanikio zaidi katika hii fani. Fatma Mussa ni muimbaji wa Dar Modern Taarab ambae kwa sasa naweza kusema nyota yake inang'aa haswaa!.
Amekuwa na bidii na juhudi katika kazi kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, hakuna alietegemea kama Fatma ipo siku moja atakuwa ni msanii anaetegemewa pale Dar Modern kwa kuweza kuimba nyimbo karibia program nzima ya bendi pasipo kuteteleka, pamoja na hayo yote lakini Fatma anasema hatosahau siku waliyosimamishwa kazi yeye na wenzie kumi na tatu, lakini anamshukuru Bosi wake Abdallah Feresh kwa kugundua kipaji chake na kumrudisha tena kazini.
FATMA MUSSA MUIMBAJI WA DAR MODERN TAARAB!. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni