TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 5 Desemba 2014

ZENA MOHAMEDY AITOSA 5 STAR'S NA KUJIUNGA OGOPA KOPA CLASSIC BENDI!.

NA KAIS MUSSA KAIS

             Muimbaji Zena Mohamedy ameamua kusaini mkataba mpya kabisa na bendi ya Ogopa Kopa Classic, na kuitosa kabisa bendi yake ya zamani ya 5 stars Modern Taarab. Zena ambae mpaka juzi alikuwepo mazoezini kwa 5 stars akitengeneza wimbo mpya ambao ilikuwa auimbe yeye, amesema ameamua mwenyewe kwa ridhaa yake kujiunga na Ogopa Kopa na wala hakuwa na mkataba na 5 stars.

ZENA MOHAMEDY MSANII MPYA WA OGOPA KOPA.
            Unajua haya ni maisha katika muziki na unatakiwa usome alama za nyakati, sina tatizo na Ally J na wala uongozi wake nawatakia maandalizi mema ya albam yao mpya lakini mimi nimehama huko sipo tena alimalizia.Baada ya Zena kuingia rasmi Ogopa Kopa, Director msaidizi wa bendi hiyo Hemedy Omary ukipenda muite "SONARA WA MANENO" amemtungia wimbo mzuri uitwao"PALIPO NA WEMA UBAYA HAUKOSI" ambao umeanzwa kutengenezwa haraka sana ili uwepo katika album hii mpya kabisa ya Ogopa Kopa Classic Bendi. Nilipompigia simu mkurugenzi wa 5 stars Ally J yeye amesema kwanza hakuwa na taarifa kama msanii wake Zena Mohamedy amejiunga na Ogopa Kopa ila kama amejiunga nao hakuna tatizo namtakia maisha mema huko Ogopa Kopa alipo sasa.

           Siku tatu zilizopita Zena
Mohamedy alikuwepo katika mazoezi ya bendi ya 5 stars akimalizia kutengeneza wimbo wake mpya uitwao "UBAYA HAUNA SOKO" ambao walikuwa wanatarajia kwenda kuurekodi siku ya jumanne ya wiki ijayo pale soundcrafters studio temeke jijini Dar. Huyo ndio Zena Mohamedy mamaa wa lauchungu halisahauliki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni