TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 5 Desemba 2014

BAADA YA ZENA KUIHAMA 5 STAR'S, SALHA WA HAMMER Q NA MAPE KIBWANA WAJIUNGA NA 5 STAR'S MODERN TAARABU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                   Usajili wa wasanii umekuwa ukiendelea kufanywa na baadhi ya viongozi wa bendi mbalimbali katika kuimarisha vikosi vyao kuelekea sikukuu za mwaka mpya na uzinduzi wa bendi zao pia.Baada ya habari kuzagaa kwamba Zena Mohamedy yupo mbioni kujiunga na bendi ya Ogopa Kopa na kuthibitika rasmi leo kupitia mtandao huu, nae mkurugenzi wa 5 star's Modern Taarab Ally J aliamua kufanya mapinduzi kwa kufanya mazungumzo na wasanii Salha Abdallah au almaarufu kama Salha wa Hammer na Mape Kibwana muimbaji wa zamani wa Dar Modern Taarab ili wajiunge na 5 stars Modern Taarab, na kufanikiwa kupata saini zao.

SALHA WA HAMMER Q, MUIMBAJI MPYA WA 5 STAR'S MODERN TAARABU!.
               Nilipoona Zena Mohamedy simuelewi, mara anakuja mazoezini mara haji nikajua wazi kwamba hapa kuna jambo linaweza kutokea sababu wasanii mimi nawajua kwani mimi mwenyewe ni msanii, ndipo nilipoanza kufanya mazungumzo na wasanii hawa kimya kimya bila yeyote kujua katika bendi zaidi ya viongozi wenzangu tu, namshukuru mungu tumeshamalizana na hawa wasanii na tayari nyimbo zao zipo, Mfano huyu Salha atapewa wimbo uitwao "KISHTOBE" na Mape Kibwana anataarishiwa shairi zuri ambalo ataliimba katika albam hii mpya ijayo

MAPE KIBWANA MUIMBAJI MPYA WA 5 STAR'S MODERN TAARABU!.
, kikubwa nawaomba wapenzi wa 5 Stars wasitetereke wala kuumizwa na kuondoka kwa Zena Mohamedy kwani tumejipanga vyema na tupo vizuri alimalizia Ally J.

            Viongozi mbalimbali wa mabendi wamekuwa wakihaha usiku na mchana kutafuta wasanii wa kuweza kufanya nao kazi katika kipindi hiki kigumu kuelekea sikukuu mbalimbali za mwisho wa mwaka zinazokuja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni