TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 5 Desemba 2014

ABDUL MALICK:- NIMEAMUA KUACHA KAZI MASHAUZI CLASSIC KWA SABABU.................

NA KAIS MUSSA KAIS


                 Habari kwamba Abdul Malick amesimamishwa kufanya kazi ndani ya Mashauzi Classic zilianza kuzagaa tokea wiki mbili zilizopita, mtandao huu uliamua kufuatilia habari hiyo kwa makini zaidi ili tuweze kuwaletea maelezo ya pande zote mbili yaani uongozi wa bendi hiyo pamoja na Abdul Malick mwenyewe ki haki kabisa bila longolongo yoyote.

            Habari hii ilipofika katika dawati letu la habari, tulimpigia simu Abdul Malick na kumuuliza juu ya kusimamishwa kwake sababu ni nini?, mwanzoni alionekana kuzungusha lakini baadae alisema kwamba amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu!, Unajua ilikuwa katika show pale mango garden naimba nipo stejini!, sasa mice niliyokuwa naimbia ilikuwa haitoi vizuri nikaita "ONE TOUCH" hii ni system ambayo tumezoea waimbaji wa Mashauzi kumuita fundi mitambo "IDDY" ili aje kuturekebishia mice kama zina matatizo, Lakini pamoja na kuita zaidi ya mara tatu jamaa hakuja kurekebisha mice niliyokuwa naimbia, nilipoona vile mimi mwenyewe nikasogea katika mixer nikajizidishia mice yangu ili niweze kusikika nini nilichokuwa naimba!.

ABDUL MALICK.
        Alipoona nimefanya hivyo akaja mbio katika mixer akaizima ile mice ambayo mimi nilikuwa naimbia, nikashangaa sana, nikaamua kuchukuwa mice ya waitikiaji ili niendelee kuimba sababu muziki ulikuwa unaendelea na watu walikuwa wanatuangalia pale stejini, nayo pia akaizima ili nisisikike, mimi nikamfuata Kali Kitimoto nikamwambia zima tu muziki ndugu yangu labda sitakiwi kuimba!.Niliposhuka stejini akanifuata "steji masta" Hashim Said na kuniambia kwamba meneja Sumalagar amenisimamisha kazi kwa muda wa wiki moja! nilishangaa pia kwanini nisimamishwe peke yangu? wakati kama makosa tumefanya wote na fundi mitambo?.

          Nikaheshimu maamuzi yake sababu yeye ni kiongozi wangu pale mashauzi, Juzi wakati wa onyesho maalum la usiku wa Isha nilikwenda mango garden nikakutana na viongozi, tukasalimiana baadae nikamtumia sms meneja Suma kuuliza ni lini adhabu yangu inakwisha maana wiki moja aliyosema ilikuwa imeshapita zaidi, matokeo yake hakuijibu ile sms yangu zaidi ya kuwaonyesha watu aliokuwa kakaa nao! sijui sababu yakuionyesha sms yangu ambayo nilimtumia kama meneja wangu ni nini anajua yeye.

         Sasa leo hii wakati nimekaa maeneo ya mwananyamala A mara naiona gari ya mashauzi classic inapita kukusanya wasanii ili kuelekea katika show mbezi, nikampigia simu dereva nikamuuliza mbona mmenipita? akanijibu hana taarifa za mimi kupitiwa kama msanii!, nikampigia steji masta Hashim Said nae akasema hajui lolote labda nimpigie meneja ambae ni Sumalagar, nilipompigia Sumalagar anasema niendelee kukaa!, ndipo nilipoamua kusema kwamba mimi na mashauzi basii inatosha maana inaonyesha kama sitakiwi katika bendi hii alimaza kwa kusema.

           Wiki moja iliyopita nilimpigia simu meneja Sumalagar ili aweze kutoa uthibitisho wa kusimamishwa kwa Abdul Malick, lakini alijibu kwamba yeye hajui lolote juu ya jambo hili!, vile vile akaendelea kusema kwamba kwani ni lazima uiandike stori hiyo mbona mashauzi wana stori nyingi tu? ni jambo la kustaajabisha sana, ila ninachoweza kumueleza meneja Suma ni kwamba huu ni mtandao ambao unaandika habari za wasanii wote wa taarabu na bendi zote za taarabu hivyo unapopigiwa simu, jaribu kutoa ushirikiano na aliekupigia ili jamii ielewe tatizo au chochote kile utakachoulizwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni