TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 5 Desemba 2014

USIKOSE USIKU WA MIAKA MINANE YA JAHAZI MODERN TAARABU, KUTAKUWA NA SURPRISE KIBAO!.

NA KAIS MUSSA KAIS

                Bendi yako ya Jahazi Modern Taarabu siku ya Jumapili tarehe 21/12/2014 inatarajia kufanya onyesho la nguvu katika kusherehekea kutimiza miaka minane tokea kuanzishwa kwake, onyesho hilo ambalo litafanyika katika ukumbi wa Travetine magomeni jijini Dar, litasindikizwa na bendi ya East African Melody na show inatarajia kuanza saa mbili usiku hadi majogoo.

MALKIA LEYLA RASHIDI AKIWA NA FATHYA, MTANGAZAJI WA VIPINDI VYA TAARABU NAIROBI.
             Siku hiyo wasanii wote ambao wamewahi kufanya kazi Jahazi Modern Taarabu kipindi cha nyuma na kwa sasa wapo katika bendi zingine watajumuika katika maadhimisho ya sherehe hizo, wadau na wapenzi mnaombwa kujitokeza kwa wingi katika sherehe hiyo ili kupongezana kwa mafanikio iliyoyapata Jahazi kwa kipindi cha miaka minane iliyopita.

        Dawati la mtandao huu tunachukuwa nafasi hii kupongeza Ideal hii kwani ni nzuri sana na itakuwa ni jambo la busara na hekima kubwa endapo na bendi zingine zitaiga mfano huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni