NA KAIS MUSSA KAIS
Mipasho katika muziki wa taarabu hapa nchini haukuanza leo, ni tangu enzi na enzi mpaka kukutia akina Nasma Hamisi kidogo ambae kwa sasa ni marehemu, pamoja na Khadija Omary Kopa malkia wa mipasho nchini tanzania.
Muziki
wa mwambao una aina kadha wa kadha.Wataalamu wa muziki wa aina hiyo
wanaweza kukuambia mengi kuhusu aina hizo na pia jinsi gani unaweza
kuitofautisha kutokana na midundo,mashairi, muonekano wa waimbaji wake
nk.
NASMA HAMISI "KIDOGO" ENZI ZA UHAI WAKE, AKIWA SAMBAMBA NA KHADIJA KOPA. |
Aina
mojawapo iliyojipatia umaarufu sana kipindi cha nyuma kidogo ilikuwa
inajulikana kama mipasho”. Neno hili mpaka hivi leo bado tafsiri yake
haiko wazi.Jambo moja ambalo lipo wazi ni kwamba kwenye muziki wa
mwambao ambao wengi wetu tunaufahamu kwa kifupi tu kama Taarab, majina
yaMarehemu Nasma Khamisi Kidogo na Bi.Khadija Omar Kopa ni majina ambayo wapenzi wa muziki huo na watanzania
kwa ujumla wanayatambua fika kwa kipindi kirefu.
Kuna wakati “upinzani” baina ya wawili hawa ulikuwa
ni kama ule wa Yanga na Simba. Jambo moja ambalo wengi tulikuwa hatujui
ni kwamba magwiji hawa wa muziki wa taarabu hapa nchini mwetu marafiki na kilichokuwa
kinatendeka kwenye majukwaa na katika mashairi ilikuwa ni hali halisi ya
usanii uliokomaa. Hivi neno “mipasho” lina maana gani?Nambeni jibu kwa anae fahamu zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni