MUSSA KIJOTI MUIMBAJI WA 5 STAR'S MODERN TAARAB. |
Bendi ambazo zitasindikiza uzinduzi huo ni pamoja na Ogopa Kopa na malkia Khadija Omary Kopa, Wakaliwao Modern Taradance, Bi Mwanahawa Ally, Jokha Kasim, Abdul Misambano, Ashura Machupa na kibao kata, Wasanii wote hao watapanda steji kwa zamu ili kuwapa burudani wapenzi watakao hudhuria uzinduzi huo bab-kubwa!.
Dawati la habari la mtandao huu linapenda kumpongeza Ally J kwa kuweza kupambana na kufanikiwa kuweza kuisimamisha tena bendi hii kwa juhudi zake zilizo thabiti kabisa. waswahili wanasema ukiwa na nia ya dhati basi utafanikiwa, wengi hawakuamini walipoona Ally J akipambana usiku na mchana katika kuinusuru bendi yake isipotee! na leo hii wamebaki midomo wazi hawaamini kile kilichopo mbele ya macho yao yaani uzinduzi wa albam ya sita...si mchezo Hongera sana kiongozi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni