TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 9 Desemba 2014

MASHAUZI CLASSIC, MSAGASUMU KUFANYA MAKAMUZI SAVOY HOTEL MOROGORO SIKU YA X-MASS!.

NA KAIS MUSSA KAIS

                 Bendi ya Mashauzi Classic chini ya Madame Isha Ramadhan wa Makongo, siku ya tarehe 25/12/2014 christimas day inatarajia kufanya show ya nguvu kwa wakazi wa morogoro na vitongoji vyake ndani ya ukumbi wa kisasa wa Savoy Hotel wakishirikiana na msagasumu kabali yao.



           Show hiyo ambayo itamaliza kiu ya wakazi wa morogoro ambao walikuwa wakiihitaji sana bendi yao ya Mashauzi Classic ikatumbuize huko inatarajia kuanza saa tatu kamili za usiku hadi majogoo kwa kiingilio chako cha shilingi 8000/= tu!. Siku hiyo Isha Mashauzi anatarajia kuimba nyimbo zake zote ambazo zinapendwa kwa sasa bila kusahau ule wimbo wake mpya kabisa uitwao SURA SURAMBI!..

           Kwa upande wa msagasumu yeye amesema kwamba huwa anajisikia raha sana pale anapopata nafasi ya kutumbuiza mkoani morogoro kwani ana wapenzi na mashabiki wengi sana wanaosapoti kazi zake. Nitawapa nyimbo zangu mpya kabisa ambazo hawajapata kuzisikia popote pale, nawaomba wapenzi wangu kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kupata burudani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni