TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 8 Desemba 2014

DAR MODERN TAARAB!, MSAGASUMU KABALI YAO NDANI YA KOPAKABANA JUMANNE TAREHE 9/12/2014!.

NA KAIS MUSSA KAIS

SIKUDHANI ALLY MUIMBAJI WA DAR MODERN.
               Bendi yako bora kwa sasa Dar Modern Taarab sambamba na Msagasumu kabali yao, Jumanne ya tarehe 9/12/2014 wanatarajia kufanya yao ndani ya ukumbi wa kopakabana mwananyamala A. Akizungumza na mtandao huu bora kabisa kwa sasa Meneja wa bendi hiyo Mr Bakari alijinasibu kwa kusema wamejipanga vyema katika kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa mwananyamala na vitongoji vyake.

            Kwa upande wa Msagasumu yeye alisema ni muda mrefu amekuwa akifanya mazoezi katika kujiandaa na burudani hiyo kwani anaamini kuwa mwananyamala ana wapenzi wengi sana wanaosapoti kazi zake, Sisi mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com tunawaahidi wapenzi kwamba tutakuwepo hapo ukumbini ili kuweza kufahamiana na wadau mbali mbali ambao wamekuwa wakisoma habari zetu mara kwa mara kupitia hapa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni