TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 7 Desemba 2014

TAMASHA LA MITIKISIKO YA PWANI MWAKA HUU:- BENDI ZAANZA KUTAMBIANA!.

NA KAIS MUSSA KAIS

                Tamasha la Mitikisiko ya Pwani mwaka huu itakuwa Bab-kubwa kuliko miaka yote kwani ushindani ni mkubwa sana kwa bendi shiriki, mazoezi au maandalizi yamekuwa ni ya hali ya juu kupita kiasi. Bendi ya Dar Modern imekuwa ikifanya maandalizi ya nguvu na imepania kuonesha makubwa siku hiyo.

          Kwa upande wa Jahazi wao wamejinasibu kwamba ni lazima wazikalishe bendi zote shiriki kwani ni kawaida yao kila mwaka kufanya hivyo, hatuna pressure sisi ndio Jahazi bendi bora tanzania. wao mashauzi Classic wamesema ni kawaida yao kufanya vizuri katika tamasha la mitikisiko ya pwani kila mwaka, wapenzi wajiandae na style mpya ambayo wataingilia stejini siku hiyo.

          Wakaliwao wamekuwa wakibuni style mbalimbali mpaka zingine za kisingeli na hii yote ni katika kuonyesha ubora wa kazi zao pindi wanapokuwa stejini, akizungumza na mtandao huu Thabit Abdul alisema anawaomba team wakaliwao kujitikeza kwa wingi siku hiyo kwani itakuwa pambe hatari.

       Malkia wa mipasho nchini tanzania bibie khadija omary kopa amejinasibu kwa kusema kikosi chake kipo fiti chini ya director Hassan Ally na watadhihirisha ni kwanini wanaitwa ogopa kopa, sisi hatumuogopi yeyote zaidi ya mungu tu, hapa kazi tu majungu huko huko kwao!.

    East African Melody wao wamesema wataifanya steji ya Dar Live siku hiyo kutikisika kwani maandalizi yao kwa ajili ya tamasha hilo ni makubwa na kama kawaida yetu sisi hatubahatishi, tunapiga kazi masihara hatuna wala kujuana siku hiyo ni NO!.

       Msagasumu amesema yeye ndio kabali yao mtoto wa uswahilini, sina ninae mhofia hata mmoja, nikipanda mimi steji watafunga vyombo vyao wakalale ni makamuzi tu mwanzo mwisho.Tamasha la mitikisiko ya pwani linatarajiwa kufanyika tarehe 13/12/2014 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar, ni tamasha kubwa kuliko yote ambayo huwa yanafanywa hapa nchini tanzania.Hongera sana ziende kwa Times redio na wadhamini wake kuweza kufanikisha tamasha hili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni