TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 7 Desemba 2014

EMANUEL KARUGILA:- WAIMBAJI WA TAARABU WAACHE MALALAMIKO JUU YA NYIMBO ZAO KUFANYWA MIITO YA SIMU!.

NA KAIS MUSSA KAIS

               Yule muhusika mkuu wa tamasha la Coast Night kwa upande wa hapa Tanzania Mr Emanuel Karugila au almaarufu mzee Imma, ameamua kufunguka kuhusu malalamiko ambayo amekuwa akishutumiwa na baadhi ya waimbaji wa muziki wetu huu wa taarabu kwamba wamekuwa wakizungushwa malipo yao yanayohusiana na nyimbo zao kufanywa miito ya simu na kampuni ya PUSH MOBILE hapa tanzania.

            Mimi huwa nawasaidia kuwapeleka tu pale PUSH sababu ni mtu ninae fahamika na menejimenti, sasa taratibu za kukabidhiana nyimbo na kampuni zinapokuwa zimewezeshwa, mimi nakuwa sina jukumu lingine tena isipokuwa issue inabakia kati ya msanii na uongozi wa kampuni juu ya malipo yake kama nyimbo inafanya vizuri ama lah!.

ZANZIBAR STAR'S MODERN TAARAB.
          Lakini cha ajabu nimekuwa nikisikia malalamiko mengi toka kwa waimbaji wa taarabu juu ya issue ya malipo ya kazi yao! na kuniingiza mimi katika tuhuma hizo, ninachoweza kusema ni kwamba wasinihusishe mimi na suala la malipo yao kikubwa wanatakiwa kwenda mpaka pale ofisini then wataelekezwa taratibu zote ziko vipi katika kuweza kulipwa haki zao, na wanatakiwa kukumbuka kuwa sio kila nyimbo ukipeleka pale PUSH basi utalipwa tu hapana!, inategemea na mahitaji ya wenye simu za mikononi je wanatumia kwa wingi huduma ya wimbo wako kama ringtone? au tokea umeupeleka upo upo tu!, kwa ufafanuzi huu sitegemei kusikia malalamiko tena dhidi yangu alimaliza kwa kusema.

T MOTTO MODERN TAARABU.

           Waimbaji wengi wa taarabu nchini wamekuwa wakisaidiwa mambo kadhaa wa kadhaa na Mr Emanuel Karugila ikiwemo kupeleka nyimbo zao katika kampuni hiyo ya miito ya simu, lakini ajabu wamekuwa si waelewa mpaka kufikia kutolewa ufafanuzi leo dhidi ya jambo hili!, ni matumaini makubwa ya mtandao huu kwamba waimbaji wa taarabu watakuwa wamemuelewa vyema muwakilishi huyu wa tamasha bora kabisa afrika mashariki na kati la Coast Night kwa upande wa hapa tanzania.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni