NA KAIS MUSSA KAIS.
Viongozi wa bendi mbalimbali za Taarab nchini Tanzania wamelalamikia utendaji mbovu tena usio na usimamizi uliotukuka kwa Baraza la Sanaa Tanzania "BASATA", juu ya bendi au vikundi vinavyoendesha shughuli za burudani kwenye Mabar mbalimbali hapa nchini tena pasipo kibali cha shughuli hiyo.
Akizungumza kwa uchungu mkubwa mmoja wa viongozi hao ambae hakupenda jina lake litajwe amesema hawa wenye vikundi uchwara ndio ambao wanarudisha nyuma soko la Taarab hapa nchini Tanzania, leo hii mtu hana haja ya kulipa kiingilio wakati akiutaka wimbo wa Sabaha Salum Muchacho anaupata Bar tena "Live" bila wasiwasi wowote ule!.
Kiongozi mwingine mwenye Jina kubwa katika tasnia hii alisema inatuuma sana sababu kama uonavyo tunatoka katika kikao chetu na moja ya ajenda iliyokuwepo ni kwa sisi kama bendi kulipia yale makato ya kila mwezi pale Baraza la Sanaa lakini wenzetu walio wengi ambao wanapiga kwenye Mabar "OPEN SHOW" kwanza hizo bendi zao hazijasajiliwa Basata, pili hata gharama za kulipa ushuru wa utendaji wa shughuli hizo hawalipi na hawazijui kabisaa!!.
Kilio chetu kwao BASATA tunaomba kupitia mtandao huu makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com waamke sasa, na waanze kusimamia haki kihalali, na kama hawawezi basi ni bora waingie ubia na mtu au kampuni ambayo itasimamia shughuli hizi kisheria zaidi, sisi tumechoka kufanywa ngazi na hawa watu. Mbona kampuni ya majembe inafanya vizuri kwa TRA? kwanini Basata washindwe? alimalizia kwa kuhoji.
Sisi kama mtandao makini wa ubuyuwataarabu.blogspot.com Tunaomba Basata kutofumbia macho malalamiko haya ya wamiliki wa mabendi ya Taarab nchini, kilichopo ni kuthubutu na kuchukuwa hatua kali kwa mabendi haya, kwani hawa wengine wanaumia na malalamiko kama haya ni mengi sana.
Jumapili, 4 Januari 2015
WAMILIKI WA BENDI ZA TAARAB NCHINI WALALAMIKIA UTENDAJI MBOVU WA BASATA!.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni