TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 7 Machi 2015

BI MWANAHAWA ALLY:- NIMEIMBA NYIMBO ZAIDI YA MIA MOJA MPAKA SASA...NYINGINE SIZIKUMBUKI!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Bi Mwanahawa Ally "jembe gumu" ni muimbaji wa muziki wa taarabu wa muda mrefu ambae amepitia bendi mbalimbali tokea visiwani zanzibar mpaka huku Dar, siku ya jana wakati bendi ya gusagusa min bendi wakitumbuiza katika ukumbi wa Max Hall ilala jijini nilipata bahati ya kuzungumza na Bi mkubwa huyu baadhi ya mambo yanayohusiana na muziki wetu huu! kwanza kabisa nilimuuliza Je mpaka sasa kwa kumbukumbu yake ni nyimbo ngapi ameweza kurekodi tokea ameanza kuimba taarab?.

BI MWANAHAWA ALLY AKIWA STEJINI.

      Nimeimba nyimbo zaidi ya mia moja tokea nianze muziki huu, pale East African Melody nimeimba zaidi ya nyimbo sabini, magereza nimerekodi, Jahazi, G5, Dar Modern, Super sonic ya unguja, Culture na bendi nyingine nyingi, wakati mwingine hata mashairi niliyoimba huko nyuma nasahau sababu ni nyimbo nyingi mno.

 UBUYU WA TAARAB:- Siku hizi kuna waimbaji chipukizi wameibukia na wanatishia nafasi zenu wakongwe katika suala zima la uimbaji, unadhani muimbaji gani umekuwa ukimhofia na kukupa wakati mgumu sana kumfikilia?.

BI MWANAHAWA:- Kwanza nawakaribisha sana katika tasnia yetu hii, pili napenda kukueleza kwamba sina ninae mhofia zaidi ya mungu pekee, alafu nafasi yangu itabaki pale pale hakuna Mwanahawa Ally mwingine zaidi yangu habari ndio hiyo!.

BI MWANAHAWA ALLY AKIFANYA YAKE.

UBUYU WA TAARAB:- Ni waimbaji gani unawakubali sana kwa uimbaji wao mpaka sasa hapa nchini?.

BI MWANAHAWA:- Waimbaji ninao wapenda haswaa ni Fatma Mahamudu, Saada Nassoro na Khadija Yusuph, hawa nawapenda sana sababu wanaimba vizuri sana mungu awaongoze na awape mafanikio zaidi na zaidi.

 Huyo ndie Jembe gumu ambalo linalima hadi kwenye lami, kwa sasa mwana mama huyu ukimtaka unaweza kuja kumuona katika show zote za Gusagusa min bendi pale ilala, magomeni na kawe.

            

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni