TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 4 Machi 2015

KHADIJA OMARY KOPA AMLILIA KAPTEN JOHN KOMBA.

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Malkia wa mipasho nchini tanzania Khadija Omary Kopa amesema kifo cha Kapten John Komba ni pigo kubwa sana kwake kwa kuwa alikuwa Bosi wake na pia ni mtu ambae walikuwa wakishauliana mambo mengi yahusuyo muziki.

KHADIJA OMARY KOPA AKIWA KATIKA MAJONZI MAKUBWA.
    Wakati mwingine unaweza ukamkufuru mwenyezimungu pale unapofikwa na msiba mzito na kusahau kuwa mungu hafundishwi na kazi yake siku zote haina makosa. Marehemu Komba ni miongoni mwa watu walionifanya mimi nikahamia Dar na kujiunga na bendi ya TOT, alikuwa akinipa ushauri nami kuufuata mpaka hapa nilipofikia!, mafanikio niliyo nayo sasa, marehemu amechangia kwa kiasi kikubwa sana alisema.

KHADIJA OMARY KOPA AKILIA KWA UCHUNGU.
    Aliendelea kwa kusema kilio changu kwake ni kikubwa mno na sina la kufanya zaidi ya kumuombea Dua ili mwenyezimungu ampe kivuli miongoni mwa vivuli vya peponi mpendwa wetu marehemu Kapten John Komba. Safari ni yetu sote ila yeye ametangulia, tuliobaki hapa duniani tusijisahau ila tujiwekee misingi bora na tujiandae kwa kifo kwani kifo huwa hakipigi hodi muda na wakati wowote hutokea.

  Hayo ndio ya malkia wa mipasho nchini Khadija Omary Kopa, lakini kikubwa tutambue dunia ni ya kupita tu hakuna atakae baki, tuache chuki hasama dharau na majivuno, hizo sifa zingine ni za mwenyewe muumba. tumuabudu mungu zaidi ili tuwe na mapokezi mema siku ya mwisho.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni