WANAUME wengi wanaojishughulisha na Muziki wa Taarab, maarufu ‘Mipasho’ huonekana wamepotea kwa kuchagua burudani inayopendwa na kinamama.
Muziki wa taarab umechangia kuongezeka kwa misamiati mingi katika miji ya pwani, na hasa Dar es Salaam, Tanga na Zanzibar ambapo kinadada huitumia kunogesha mazungumzo wenyewe huita ‘kupashana.’Lakini wengi hawafahamu kuwa muziki wa taarab ulipofika pwani ya Afrika Mashariki katika karne ya 19, mjini Unguja, wanawake hawakuruhusiwa kuimba, kupiga vyombo wala kucheza muziki huo.
Kumbukumbu na historia kuhusu muziki wa taarabu, zinasema aliyeleta burudani hii katika Afrika Mashariki, ni Sultan Seyyid Baraghash Bin Said ambaye alitawala Zanzibar kati ya mwaka 1870 na 1888.
Inadaiwa kwamba Sultan huyo alikuwa akipenda sana muziki huo, na kwa hiyo akawa anaagiza vikundi vya burudani hiyo kutoka Misri ambapo wanaume tu ndio waliokuwa wakiimba na kupiga ala zote katika jumba la starehe la Beit El-Ajaib.Kwa mujibu wa kumbukumbu hizo, Mzanzibari wa kwanza kuonyesha uwezo wa kuimba taarab anatajwa kwa jina la Mohammed Ibrahim. Huyo alikuwa Mzanzibari wa kwanza kupelekwa Misri na Sultan Seyyid Bin Said kujifunza kuimba taarab na kupiga ala za muziki huo ili akiweza aje kuwafundishe wengine na hivyo kumpunguzia gharama Sultan huyo ya kuagiza vikundi kutoka Misri kila anapohitaji.
Inaelezwa kwamba Ibrahim, akiwa Misri, alijifunza kupiga chombo cha Ganuni (Gannon) ambacho ni chombo kigumu kujifunza kuliko vyote kwenye muziki wa taarab. Ganuni ni mfano wa kinanda chenye nyuzi za waya. Hadi sasa inasemwa kwamba ni wanamuziki wachache mno wanaojua kucheza chombo hicho.
Baada ya kuhitimu mafunzo hayo, Mohammed Ibrahim alirudi Zanzibar na kuanza kuwafundisha Wazanzibari wenzake kuimba na kupiga vyombo vya taarab, kabla ya kuanzisha kikundi cha kwanza cha taarab katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kilichojulikana kwa jina la Zanzibar Taarab Orchestra.
Baadaye jina la kikundi hicho lilibadilika na kujiita Zanzibar Cultural Musical Club, jina ambalo hadi leo lipo Visiwani lakini sasa kikundi hicho kikijulikana kama kikundi cha taifa. Aidha kikudi hicbo sasa kinatumika kama chuo cha taarab pale mjini Unguja.
Mwaka 1905, kikundi cha pili cha taarab kilianzishwa kwa jina la Nadi Ikhwani Swafaa. Kwa kuwa na vikundi viwili hivyo vilivyokuwa vikishindana kumburudisha Sultani na ukoo wake, gharama tena ya kuagiza vikundi kutoka Misri ikawa imeokolewa. Vikundi vyote hivyo viwili vya taarab vilikuwa na wanamuziki wanaume tu, kwa kuwa wanawake hawakuruhusiwa.
Miaka ya 1920 mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kukata minyororo ya utumwa na kupaza sauti kwa uimbaji taarab alikuwa ni Bi Mtumwa Saad, maarufu kwa jina la Sitti Bint Saad. Ikumbukwe pia kwamba miaka hiyo, taarab ilikuwa ikiimbwa kwa lugha ya Kiarabu, ingawa Kiswahili kilitumika kwa kiasi kidogo.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za nyaraka zilizopo, mashairi ya nyimbo za muziki huo yaliandikwa kwa hati za Kiarabu, lakini yakisomeka kwa lugha ya Kiswahili. Hii ilikuwa kasumba ya Waarabu kwani iliaminika asili ya muziki huo ni lugha ya Kiarabu hivyo kutumia lugha nyingine ilikuwa ni kama kuupunguzia ladha.
Ikumbukwe pia kwamba muziki huo wa taarab ulitumika kuwaburudisha mabwanyenye wa Kiarabu ambao wengi wao walikuwa ni kutoka ukoo wa Kisultani. Ulitumbuizwa katika kasri la Sultani tu, na wala haikuruhusiwa kupigwa mitaani, yaani haukutumika kwa kupata kipato kama inavyofanyika sasa.
Sitti Bint Saad huyo huyo, anatajwa kuwa mtu wa kwanza kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki kurekodi sauti yake, akiimba taarab nchini India katika studio moja maarufu kwa wakati huo, iliyokuwa ikijulikana kwa jina la ‘His Master’s Voice,’ ingawa baadhi ya vitabu vimeitaja studio hiyo kwa jina la Kampuni ya Columbia Records.
Mpaka sasa jina la Sitti Bint Saad aliyefariki dunia Juni 1950, halijasahaulika midomoni mwa wapenzi wa taarab kwani ndiye huyo aliyewakomboa wanawake kutoka kwenye marufuku ya kuimba na kupiga zana za muziki huo, kiasi leo hii taarab sasa inaonekana na muziki unaopaswa kuimbwa na mwanamke na inapotokea kwa mwanaume kufanya hivyo anaonekana wa ajabu kama ilivyokuwa a
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni