TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 9 Machi 2015

WAJUE NEW GOLDEN STAR MODERN TAARAB, TOKEA MKOANI TANGA. MAFUNDI WA TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

          Leo ninaendelea kuwajuza bendi ya pili ambayo nilifanikiwa kufanya nao mahojiano wakati nilipokuwa mkoani Tanga nayo si nyingine ila ni "New Goldenstar Modern Taarab", Bendi hii ina historia kubwa sana, na kwa wapenzi wa muziki huu na hususani wakazi wa Tanga wanalitambua hilo.

  Hapo mwanzoni ilikuwa ikifahamika kama "Goldenstar Music Club" ni moja ya bendi kongwe za mkoa wa Tanga. kipindi hicho bendi hii ilikuwa ni miongoni mwa bendi zenye upinzani mkubwa na bendi zingine za mkoa huo kama vile Freedom,Babloom,Blackstar,Luckstar na nyingine nyingi zilizotamba miaka nyuma.

   Kwa sasa imeongezewa neno "New" ili kwenda na wakati zaidi hususani karne hii ya sayansi na teknorojia, niliweza kufanya mahojiano na mkurugenzi wa bendi hii Mr Amour Kassim, kwanza kabisa nilitaka kujua mpaka sasa bendi hii ina wasanii wangapi?.

 AMOUR KASSIM:- Bendi hii ina wasanii kumi na mbili "12" ingawa wengine wanaishi Dar, lakini kama ujuavyo Tanga sio mbali na Dar hivyo tunapokuwa na kazi basi wasanii hawa huripoti mapema. Wasanii wa New Goldenstar Modern Taarab kwa sasa ni:-

                                1. Amour Kasim- Mkurugenzi wa bendi.

                                2. Majengo Mussa-Mwenyekiti wa bendi.

                                3. Jumaa Shilingi-Katibu wa bendi.

                                4. Hassan Baruti- Meneja wa bendi.

                                5. Abuu Mgeni- Bendi Master.

                                6. Sadiki Hassan- Bendi Master Msaidizi.

                                7. Amina Saray- Mamaa wa Nidhamu.

                                8. Shillingi Jumaa- Muimbaji.

                               9. Nzige Mwasango- Muimbaji na meneja masoko.

                               10. Salama Sambwanda- Muimbaji.

                               12. Asia Mariam "Utamu"-Muimbaji.

   Bendi hii mpaka sasa ina albam mbili, na watunzi tunaowategemea katika bendi yetu ni Profesor Hamza Ally na Profesor Jitihada, katika hizo albam mbili, Profesor Jihada katunga nyimbo 7 na nyingine 5 katunga Profesor Hamza Ally. Baadhi ya nyimbo na waimbaji wake ni:-

ASYA MARIAM, MUIMBAJI AMBAE NAE AMETAJWA KUWEMO KATIKA BENDI HII.

                             1.Kwa mimi na wewe- Jumaa Shilingi.

                             2. Haraka Rejea-Jumaa Shilingi.

                             3.Moyo ungali wapenda- Jumaa Shilingi.

                            4. Umenihasimu ghafla mpenzi- Nzige Mwasango.

                            5. Bure yenu Mahasidi-

                            6. Mpenzi Husikitiki-

                            7. Nakupa Hakika ewe wangu nyonda-

  Hizi ni baadhi tu ya nyimbo zilizokuwemo katika albam hizo mbili, vile vile mwishoni mwa mwezi wa nne, bendi yangu natarajia itakuwa inamiliki vyombo vipya kabisa ambavyo thamani yake ni pesa za kitanzania milioni kumi na tano, 15, 000, 000/=.

 UBUYU WA TAARABU:- Nimepata taarifa kwamba kuna baadhi ya wasanii wamejiengua katika bendi yako akiwemo Bi Mwanaela unadhani nini sababu ya kukuacha?.

 AMOUR KASSIM:- Uchakavu wa vyombo umechangia kwa kiasi kikubwa wasanii kuondoka katika bendi yangu ndio maana nikaagiza seti ya vyombo vipya kabisa ili kwenda sambamba na soko la ushindani ambalo kwa sasa mkoani Tanga limekuwa likikuwa kila kukicha. Vile vile bendi itakuwa na safari ya Dubai na mungu akipenda tutaenda na wasanii wanane "8" kulingana na waliotualika na idadi waitakayo.

  Kilio kikubwa cha bendi zote za Tanga ni kupata wafadhili ili kuweza kusaidiana na kuboresha maisha ya wasanii, mimi nasema kwa bendi yangu milango kwa wafadhili ipo wazi kabisa.

  Kama una lolote unataka kuwaambia "New Goldenstar Modern Taarab toka mkoani Tanga basi unaweza kufanya nao mawasiliano kwa namba zifuatazo:- 0715-480922, 0685-909099, 0714-973288,0652-520914, 0715-395025.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni