TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 11 Machi 2015

MKURUGENZI WA GUSAGUSA ASHUTUMIWA KUFUKUZA WASANII KATIKA BENDI YAKE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Baada ya kuandika habari za mkurugenzi wa Gusagusa Min Bendi Hassan Farouk siku mbili zilizopita katika mtandao huu tukielezea mafanikio ambayo ameyapata katika uongozi wake mpaka sasa, msomaji mmoja aitwae "Ilham Majidy" mtanzania aishie Muscat, alituandikia malalamiko yake yanayomuhusu mkurugenzi huyu na kutulaumu kwanini pia hayo hatukuandika?.

      Nasi tukamuahidi kwamba tutafuatilia, ikiwemo kumuhoji kiongozi huyu na kuleta hapa hapa mbele ya wananchi na wadau wetu wapendwa. Naam siku ya jana jioni dawati la mtandao huu lilimtembelea mkurugenzi huyu nyumbani kwake magomeni mikumi jijini Dar na mazungumzo yetu yalikuwa hivi:-

MKURUGENZI WA GUSAGUSA MIN BENDI HASSAN FAROUK.

UBUYU WA TAARAB:- Mkurugenzi habari za muda huu!, tumerudi kwako baada ya kupata shutuma zako kutoka kwa wasomaji wetu kuwa umekuwa na tabia za kufukuza wasanii pindi wanapokukosea, je kuna ukweli wowote juu ya taarifa hizi?.

 HASSAN FAROUK:- Sikweli kwamba nafukuza wasanii ovyo na pasipo sababu za msingi, msanii yeyote ambae ameondolewa katika bendi hii basi ni wazi amefanya makosa na viongozi tumeshindwa kumvumilia.

UBUYU WA TAARAB:-  Ni aina gani ya makosa ambayo msanii akiyafanya kwenu viongozi basi haina budi kumfukuza bendi?.

 HASSAN FAROUK:- Makosa yapo mengi siwezi kuyaorodhesha, lakini pia tuna taratibu zetu katika bendi msanii anapokosea huwa anaonywa zaidi ya mara mbili, akirudia mara ya tatu huwa tuna msimamisha kwa muda wa wiki mbili, hii ina maanisha kama msanii atagundua makosa yake basi ndani ya wiki hizo mbili ni lazima ataandika barua ya kuomba radhi kwa viongozi na bendi kumrudisha kazini, hakuna msanii ambae huwa anafukuzwa moja kwa moja.

 UBUYU WA TAARAB:- Kuna baadhi ya wasanii tumetajiwa kwa majina kwamba umewafukuza kabisa katika bendi, mfano Salma Kasim, Sihaba Alawi na Fatuma Kidude je ni kweli mkuu?.

HASSAN FAROUK:- Wasanii wote ambao umetajiwa walikuwa wamefanya makosa na taratibu zikatumika kuwaonya, sasa unapoona msanii anajiona yeye yupo juu zaidi ya viongozi wake, basi huyo hafai kuwa nae kinachotakiwa unamfungulia milango akatafute ridhiki sehemu ingine. Kuna baadhi ya wasanii wapo Gusagusa tokea imeanzishwa mpaka sasa hawajawahi kusimamishwa wala kufukuzwa bendi mfano Bi Afua Suleiman, Khadija Kibaiya na Ally.

 UBUYU WA TAARAB:- Kwahiyo kwa shutuma hizi ulizoshutumiwa unawaambia nini wasomaji wa mtandao huu na wapenzi wa bendi yako ya Gusagusa Min Bendi kwa ujumla?.

 HASSAN FAROUK:- Ninachowaambia ni kwamba wasipende kusikiliza maneno ya mitaani yasiyo na ukweli wowote, hizo habari sio kweli ila watu wachache wanapanga njama za kutuchafua ila nawaambia kwamba kamwe hawatoweza kwani Gusagusa tupo makini sana na tunajitambua.

Hayo ndio yalikuwa mahojiano na mkurugenzi wa bendi ya Gusagusa ni matumaini yetu kwamba mtakuwa mmefaidika kwa kiasi kikubwa sana kwa majibu hayo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni