Leo Jumatano tarehe 8/4/2015 ndio rasmi tunaanza ile sagment yetu mpya kabisa inayotambulika kwa jina la "Sindano tano za Ubuyu", hapa msanii anaulizwa maswali kulingana na maisha yake binafsi pamoja na sanaa kwa ujumla. Na aliebahatika kufungua kipengele hiki kwa siku ya leo ni mkurugenzi wa Wakaliwao modern taradance Thabit Abdul au ukipenda muite mkombozi.
GARI AINA YA "BREVIS" AMBAYO INAMILIKIWA NA THABIT ABDUL KWA SASA. |
Kwanza aliponiona alipatwa na mshituko mkubwa akijua kwamba sasa hapa hakuna usalama tena kulingana maswali yangu ambayo nimekuwa nikimuuliza kila ninapopata nafasi ya kufanya mahojiano nae. Mkombozi usiogope! nilianza kwa kumpoza!, nimekuja kufanya mahojiano na wewe na naomba unijibu maswali yangu matano tu katika kipengele kipya kabisa cha "Sindano tano za Ubuyu".
1. Kuna taarifa kwamba thamani zako za ndani zote umempatia Asya mariam baada ya wewe kuhamia mikocheni katika makazi mapya!, jambo linalotafsiriwa na makachero wetu kwamba unauhusiano wa kimapenzi na msanii wako huyo...Je hili ni kweli?.
THABIT ABDUL:- Kwanza si kweli kuwa mimi nina uhusiano wa kimapenzi na Asya mariam, huyu ni msanii wangu tu kama walivyo wengine, na issue ya kumpatia vyombo vyangu vya ndani ni kweli, lakini sikumpatia yeye peke yake, niligawa kwa baadhi ya wasanii wangu, na hata Abdul malick wa Mashauzi classic nimempatia Tv pia!.
NDIVYO INAVYOONEKANA KWA NDANI |
2. Walimwengu wanasema kwamba vile vyombo vya muziki ulivyotangaza kwamba umenunua kwa pesa yako, si kweli ila ni msaada uliopewa baada ya kulialia sana kwa bosi mmoja nguli sana hapa nchini...Je ni kweli?.
THABIT ABDUL:- Mimi kuandamwa nimezoea kaka, hawakuanza leo hao, vile vyombo ni vyangu na ni jasho langu nikishilikiana na wasanii wangu, ndio maana niliweka mpaka risiti niliyonunulia katika mitandao ili watu waone, tumejinyima sana mpaka kupata vyombo vile mkuu.
3. Unafikili ulikuwa sahihi kukataa mamilioni ya pesa toka kwa mmiliki wa utalii bendi ili uungane nao?
NDIVYO INAVYOONEKANA ENEO LA DASHIBODI NA USUKANI. |
THABIT ABDUL:- Yes! nilikuwa sahihi kukataa pesa zile, kwani ni mambo mengi tunafanya mimi na mmiliki wa Utalii, pia isingekuwa kitu kizuri kuiacha bendi yangu ya Wakaliwao na kuhamia huko. Ninachofanya sasa ni kushirikiana na utalii katika kutengeneza nyimbo mpya na kuandaa show zao wenyewe.
4. Nakuona upo katika gari ya kifahari aina ya "Brevis", hebu wajuze wadau wa blog hii thamani yake haswa ni kiasi gani kaka?.
THABIT ABDUL:- Haha haha haaaa!!, kawaida sana kiongozi, hii gari ina thamani ya shilingi milioni "15" za kitanzania ndugu yangu.
5. Mwisho kasi ile ya mwanzo iliyokuja nayo bendi yako ya Wakaliwao sasa imepungua sababu haswa ni nini? au kwakuwa unafanya sana kazi za Utalli bendi na kuisahau bendi yako?. kumbuka kuwa kalamu mbili zilimshinda fisi!.
HII NI ENGINE YA GARI HIYO AMBAYO INAMILIKIWA NA THABIT ABDUL |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni