TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 15 Aprili 2015

JE WAJUA KUWA HAMISI SLIM NA WARDA MAKONGWA WA PLANET FM MOROGORO NI WAPENZI?.



NA KAIS MUSSA KAIS.

                 Asalaam aleykum wasomaji wangu wapendwa wa page hii pendwa ya "Sindano tano za ubuyu wa taarab", hapa utapata kufahamu maisha ya msanii, kiongozi au mdau yeyote wa taarab akijibu maswali matano muhimu ili upate kumfahamu na kumjua kiundani zaidi.

 

   Leo katika kipengele hiki tunae mkurugenzi wa bendi ya G5 modern taarab ndugu Hamisi Slim, kama ilivyoada nilimfuata ofisini kwake ili kutaka kujua mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakisemwa na baadhi ya watu juu yake. Na mazungumzo yetu yalikuwa ikama ifuatavyo:-

MKURUGENZI WA BENDI YA G5 MODERN TAARAB HAMISI SLIM.

UBUYU WA TAARAB:- Hamisi Slim kwanza kabisa pole na kazi za kutwa nzima, nimekuja ofisini kwako nia ni kufanya mahojiano na wewe mkuu, kuna tetesi zimezagaa mjini kwamba brother unatoka kimapenzi na mtangazaji wa Planet Fm ya mkoani morogoro anaetangaza kipindi cha taarab aitwae "Warda Makongwa" je ni kweli kiongozi?.

 

HAMISI SLIM:- Haha haha haaaa! duuh! kaka wewe mbona chimbuchimbu sana mkuu? ukweli ni huu, sio kwamba natoka nae kimapenzi tu!, Warda makongwa ni mchumba angu na familia zote mbili zinatambua hilo na tupo katika mipango ya kufunga ndoa, Naomba jamii nzima itambue jambo hili.

ANAITWA WARDA MAKONGWA MTANGAZAJI WA PLANET FM, AMBAE NI MCHUMBA WA HAMISI SLIM.

UBUYU WA TAARAB:- Hongera sana kiongozi kwa hilo!, Eehee! unauzungumziaje ule uzinduzi wa bendi yako na albam ulioufanya pale travetine, kuna tetesi kwamba ulizima simu ili kuzikwepa bendi za Extra bongo na East african melody ambazo zilisindikiza uzinduzi huo kwa madai ya kutaka kuwazungusha juu ya malipo ya pesa zao za kazi ni kweli?.

 

HAMISI SLIM:- Hilo sio kweli kaka, niliwalipa pesa zote kupitia kwa meneja wangu, sasa kama walikuwa hawajakamilishiwa mimi sifahamu, ninalojua kila kitu nililipa vizuri, na lile tukio lilifanya nimuwajibishe meneja wangu sababu sikuona haja ya kuwa nae huku akiendelea kunirudisha nyuma kimaendeleo na kunitia hasara katika bendi yangu.

HII NDIO GARI AINA YA "MARK X" AMBAYO ANATEMBELEA HAMISI SLIM KWA SASA.

UBUYU WA TAARAB:- Naona hapo nje umepaki gari ya kifahari kiongozi ni aina gani ya gari hii ndugu yangu?. Na linathamani ya kiasi gani show room?.

 

HAMISI SLIM:- Hii gari ni "Mark X" ndio naitumia kwa sasa, na show room imesimama milioni 25 hadi 26, ila nina mpango wa kununua gari ingine ambayo kiukweli naipenda sana ni prado ya kisasa, ila hata nikiinunua hiyo gari mpya, sitoiuza hii niliyonayo!.

 

UBUYU WA TAARAB:- Kuna maneno yapo mtaani kwamba bendi yako ya G5 imekufa kama zilivyokufa bendi zingine, na mpaka sasa hamna show yoyote mnayofanya je ni kweli mkurugenzi?.

HUU NDIO MUONEKANO WAKE KWA NDANI.

HAMISI SLIM:-Nimefurahi sana kuniuliza swali kama hilo, bendi ya G5 modern taarab ipo na itaendelea kuwepo daima, kuna mipango ipo chinichini maboresho makubwa yanakuja, kuanzia uongozi mpaka wasanii wapya wenye majina makubwa watasainishwa, na kambi ya mwezi mmoja tutaweka nje ya mkoa wa Dar wadau nawaomba wavute subira vitu vizuri vinakuja.

 

UBUYU WA TAARAB:- Mwisho kabisa naomba unithibitishie ni kweli kwamba  Hassan Vocha muimbaji wa Dar modern ambae hapo kabla alikuwa G5 modern taarab upo katika mipango ya kumrudisha tena kundini?.

 

HAMISI SLIM:- Hassan Vocha hapa ni nyumbani kwake, sababu wakati anatoka kwa Saidi Fellah mkubwa na wanawe alifikia hapa nadhani kurudi kwa Hassan Vocha ndani ya G5 modern taarab haitokuwa jambo la kushangaza sana.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni