TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 6 Aprili 2015

MARIAM AMOUR WA JAHAZI MODERN TAARAB AFIWA NA MUMEWE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

     Muimbaji Mariam Amour wa Jahazi modern taarab amefiwa na mumewe mpendwa anae tambulika kwa jina la "J Four" usiku wa kuamkia jana huko tegeta nje kidogo ya jiji la Dar, kwa mujibu wa  msanii mwenzake ambae wanaishi pamoja huko huko magomeni Shinuna Kasimu wa bendi ya 5 stars modern taarab ambae ni mdogo wa Jokha Kassim aliuambia mtandao huu kuwa ni kweli Mariam amefiwa na mumewe.


MARIAM AMOUR AKIIMBA STEJINI.

     Chanzo haswa cha kifo chake ni kwamba marehemu siku hiyo alikuwa akirudi mida ya usiku huko tegeta ambapo inaonekana ni kwao au kwa ndugu zake, kwa bahati mbaya baadhi ya watu wakahisi ni kibaka au kwa lugha nyingine mwizi, na kuanza kumpigia kelele za mwizi, raia wenye hasira wakajitokeza na kuanza kumpiga mpaka kuwa mahututi.

MARIAM AMOUR AKIWAPAGAWISHA WAPENZI WAKE.

   Mtoa habari anaendelea kwa kusema marehemu alikimbizwa hospitali akiwa hai ila ana hali mbaya sana, kwa bahati mbaya alipoteza maisha akiwa hapo hapo hospitali. msiba huu upo Yombo Abiola, na mpaka tunakwenda mitamboni walikuwa bado hawajazika ila taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa. Mtandao huu ili kujilidhisha zaidi na habari hii ulijaribu kupiga simu ya Mariam Amoour mwenyewe lakini haikupatikana, ndipo tulipompigia simu mussa wa udongo au Baba Warda mpiga gitaa la besi wa Jahazi modern taarab kama anavyojulikana ndani ya bendi hiyo, Yeye alidhibitisha  kwamba ni kweli msanii mwenzao Mariam Amour amefiwa na mumewe.

  Mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com tunatoa salamu za pole na rambirambi kwa Mariam Amour kwa kuondokewa na mumewe kipenzi kwani kufiwa na mume au mke ni uchungu mkubwa sana, na kwa namna yoyote ile sisi ubuyu wa taarab tutakuwa nae bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu alichonacho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni