TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 25 Mei 2015

BISHARA ADEN WA PWANI FM MOMBASA 104.7...NI HABARI YA MJINI MOMBASA NZIMA!.


NA KAIS MUSSA KAIS.
      +255657036328

             Ni jumatatu nyingine tena tumekutana katika kipengele chetu cha mjue mtangazaji wako hapa hapa katika blog bora kwa muziki wa taarab afrika mashariki na kati ubuyuwataarabutz.blogspot.com, leo tunae mwanadada mrembo toka mombasa kenya katika redio ya "Pwani Fm" 104.7. ambae anafanya kipindi cha taarab kiitwacho "Kwa raha zangu" kila siku ya jumatatu mpaka ijumaa kuanzia saa saba mchana hadi kumi kamili ambae anakwenda kwa jina la Bishara Aden a.k.a. Toto juu ya hewa!.


BISHARA ADEN "TOTO JUU YA HEWA" AKIWA KAZINI.

         Kwanza nilitaka kufahamu elimu yake aliipatia wapi?, nae alianza kujieleza:- kiukweli elimu yangu imeanzia chekechea kama wengi wanavyofahamu, nilifunzwa na mama yangu mzazi chekechea na mpaka sasa mama ni mwalimu wa "Fadhil Adhim" iliyopo mtaa wa bakarani eneo la bunge la kisauni kaunti ya mombasa mwaka 1992 nikasoma shule ya msingi papo hapo hadi darasa la nane ambapo nilifanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane mwaka 2004.


UBUYU WA TAARAB:- Bishara wewe ni raia wa kenya au ni raia wa Tanzania, maana tumekuwa tukiona raia wa nchini hizi mbili wamekuwa wakifanya kazi bila vikwazo kwa pande zote mbili, na vipi umeolewa na una watoto wangapi?.

BISHARA ADEN AKIRIPOTI HABARI NDANI YA PWAN FM 104.7 MOMBASA.

BISHARA ADEN:- Haha haha haaa!, mimi najivunia kuwa mkenya japo mama yangu mzazi ni mtanzania lakini kwakuwa nimekuwa nikijiona katika ardhi ya kenya basi mimi ni mkenya tu! lakini Tanzania naipenda sana na ndio maana kila ninapopata likizo kazini ni lazima nitembelee huko kwenu.


UBUYU WA TAARAB:- Wasomaji wangu wangependa kujua safari yako ya uandishi wa habari umepitia wapi na wapi na chuo kipi umesomea taaluma hii ya utangazaji?.


BISHARA ADEN AKIWA KWENYE POZI.

BISHARA ADEN:- Baada ya kumaliza kidato cha nne mwaka 2008 nilitaka kusoma kozi ya udaktari lakini kutokana na majibu ya mtihani wangu hayakuridhisha nilijikuta nikishindwa kusomea kozi hiyo niliyokuwa naipenda sana, nilikata tamaa nisijue nini cha kufanya ndipo mama akanishauri nijaribu kusomea kozi ya utangazaji, nikamsikiliza alafu nikajiunga katika chuo kiitwacho "Mombasa aviation training instute" ambacho kipo mombasa pia. Nilianza kwa kumtanguliza mungu sababu nilisomea kozi ambayo sikuwa naipenda, basi nikasoma mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu nikaona hii kozi imeanza kuniingia sasa damuni nikaanza kujenga tabia ya kusikiliza redio na kuangalia televisheni hadi nikamaliza mtihani wangu wa kwanza wa Certificate ambao niliufanya baada ya mwaka mmoja. Ikafika wakati wa kufanya attachment na ndio nikaanza attachment yangu ndani ya Pwani Fm redio, baadae nilijiendeleza hadi Diploma, ilipofika mwaka 2010 nikajiunga rasmi na redio pwani fm.


BISHARA ADEN WA PWANI FM MOMBASA KENYA.

UBUYU WA TAARAB:- Ni kwanini ulivutiwa kutangaza taarab na isiwe vipindi vingine vya kijamii au siasa na teknorojia?.


BISHARA ADEN:-Kwanza kabisa nilipoanza sikuwa natangaza taarab kabisa, nilikuwa ripota wa habari na mtangazaji wa taarifa ya habari, ikatokea siku moja mtangazaji wa kipindi cha taarab hakuweza kufika kazini ndipo nikateuliwa mimi nikamshikie kwa muda tu!, lakini baada ya hapo nilipata pongezi nyingi sana toka kwa watangazaji wenzangu na viongozi kwamba nimefanya vizuri kipindi, basi tokea siku hiyo menejimenti ikaniteua mimi kuendesha kipindi hiki mpaka sasa.


UBUYU WA TAARAB:- Ni watangazaji gani wa taarab ambao huwa unavutiwa nao kuwasikiliza, huko kenya na hata hapa Tanzania kama wapo unaweza kuwataja!.


BISHARA ADEN AKIJIANDAA KUANZA KIPINDI.

BISHARA ADEN:- Yah! wapo wanaonivutia na marafiki zangu sana tu akiwemo Juma Mdoe wa Kaya Fm, Tatu Amani wa Bahari Fm na Aisha Saggaf wa Taifa Fm, kwa huko Tanzania siwezi nikaweka wazi sababu sio sana kuwasikiliza kutokana redio zao hazifiki huku kwetu Mombasa. uliniuliza kuolewa, ni kwamba sijaolewa, mtoto sina wala sina mchumba, nipo mwenyewe tu nasubiria rehema ya mungu.


UBUYU WA TAARAB:- Unaizungumziaje taarab kwa huko kenya, mbona mwamko wake upo chini sana haswa kwa mabendi? tatizo haswa lipo wapi kwa mtazamo wako?.


BISHARA ADEN:- Tatizo ni ujuaji mwingi wasanii wa hapa na ma-director, wapiga vinanda wanajifanya wajuaji mno hawataki kufuata ushauri wa wadau na ma-presenter, yupo msanii mmoja tu ambae namkubali na anafuata ushauri ukimueleza jambo huyu ni " Dokta Malick" na ndio nyimbo zake zinafanya vizuri huku na hata huko Tanzania.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni