TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 23 Mei 2015

TWAHA MALOVEE:- NIPO MSONDO NGOMA...LAKINI KUIMBA TAARAB ALINIFUNDISHA MAREHEMU AHMED MGENI.


NA KAIS MUSSA KAIS.

           Wapenzi wasomaji wangu wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com ni jumamosi ingine tena tumekutana katika kipengele chetu cha "mjue msanii wako" kama kawaida, na leo tupo na Twaha mohamedy manyanga au kwa jina la kisanii anajulikana kama "Twaha Malovee" muimbaji wa zamani wa Dar modern taarab ya jijini.


TWAHA MALOVEE!.

        Nilianza kwa kutaka kujua historia yake kimaisha haswa ikoje? ndipo alipoanza kwa kusema Mimi jina halisi naitwa Twaha Mohamedy Manyanga, hili jina la Twaha Malovee ni jina la kutafutia ugali tu kiongozi, nimesoma shule ya msingi na sekondari pale vigwaza mkoani pwani, mimi ni mtoto watatu kuzaliwa kati ya watoto watano wa baba yangu mzee "Mohamedy Manyanga"  na nilifanikiwa kumaliza sekondari mwaka 2005, lakini wakati nasoma shule ya msingi ilikuwa ni msomaji mzuri wa Quraan pale madrasan kwetu, ila nilipokuwa nimemaliza tu sekondari nilikuja Dar na kuacha madrasa!.


    Nilipofika Dar nakumbuka nilikutana na marehemu Ahmed Mgeni wakati huo akiwa pale zanzibar star's nikamwambia Brother na mimi natamani sana kuimba, nae hakuwa na hiyana alianza kunifundisha njia za uimbaji wa muziki wa taarab, haikuwa ngumu sana kwa mimi kujua haraka sababu hata madrasani kwetu mimi ndio nilikuwa msoma kaswida mzuri tu! Nilianza kwa kuimba nyimbo kama mazoea yana tabu, Nipepee na nyinginezo, siku moja moja marehemu Ahmed Mgeni alikuwa ananichukua tunakwenda katika show za zanzibar srar's na ananipandisha steji nakuimba nyimbo nyepesi nyepesi japo kiuoga uoga!.


TWAHA MALOVEE AKIWA KWENYE POZI.

    Bendi yangu ya kwanza kufanya kazi ni Samsuri modern taarab ambapo sikukaa sana nikajiunga na T.M.T. modern taarab iliyopo tandale, bendi zote hizo sikufanikiwa kurekodi wimbo hata mmoja ndipo mwaka 2009 nikajiunga na Dar modern taarab chini ya mkurugenzi Abdallah Feresh. pale nilirekodi nyimbo tatu ambazo ni 1. Amali njema 2. Usimdharau mtu. 3. Penzi ajali na wimbo huu niliufanyia hadi shooting ya video.


 Wakati nipo Dar modern taarab nilikuwa nikienda pia Mapacha watatu nikawa naimba Dansi, mimi huwa napenda kujifunza zaidi, watu wakapeleka maneno ya umbea kwa Bosi kwamba nina mpango wa kuhama bendi ya Dar modern kitu ambacho hakikuwa kweli. Uongozi wa Dar modern ulipobadilishwa na kuingia akina Adam Mlamali, mimi nikaona ni bora nijiengue na kwenda zangu msondo ngoma baba ya muziki ambapo nipo mpaka sasa!, Alipoingia Mlamali alianza ubaguzi kwa kuwapendelea wanamuziki ambao amekuja nao yeye hivyo mimi kwakuwa najitambua kuwa nina uwezo wa kuimba hata dansi nikaamua kuondoka zangu, ila taarab naipenda sana na ipo damuni mwangu, huwa nakwenda pale Gusagusa na Aljazeera naimba then naondoka kwangu kupumzika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni