TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 28 Juni 2015

MADIRECTOR WA MUZIKI WA TAARAB, TUMECHOKA KUSIKIA VIPANDE VYA MUZIKI WA DANSI KWENYE NYIMBO ZENU!.


NA KAIS MUSSA KAIS.
      +255657036328

          Muziki wa taarab umekuwa ukijizolea umaarufu karibu kila kukicha, watu wa lika mbalimbali wamekuwa wakivutiwa sana na mirindimo ya muziki huu mpaka kupelekea kuikacha miziki mingine na kushabikia zaidi muziki huu wenye asili ya pwani.


     Lakini kumekuwa na kasumba ya waongozaji wa muziki huu "ma-director" kuweka vipande vya dansi au hata gospel ndani ya nyimbo zao za sasa, hii inaonyesha wazi hawana jipya na hawawezi kubuni kitu kizuri toka ndani ya ubongo wao mpaka kikapendwa badala yake wanahamisha tu bila aibu!, kuna mifano iliyo wazi kabisa katika bendi zote za taarab mpaka hizo wanazoziita kubwa wamekuwa wakikopi na kupesti. Wakati mwingine hufanya ujanja na kuiga labda gitaa la solo la bendi fulani ya dansi, wengine huiga uimbaji, wenzangu na mimi nao wamekuwa wakiiga mpaka style ya kurap hii hatari sana taarab mnaipeleka wapi?.


    Siku moja nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambae ni muimbaji wa Fm Academia nisingependa kumtaja jina, nikajaribu kumuuliza nini maoni yake juu ya muziki wa taarab?, yeye alinijibu kwamba taarab hawana jipya kila siku mirindimo yao ni ile ile tena inafanana, hawana uwezo wa kubuni kitu kipya wamekuwa wakidumaa kiakili kila kukicha!, yaani muziki wa taarab unajua kabisa baada ya introduction atafuata muimbaji, baadae wataitikia mwisho watamalizia na ngoma chini! yaani wamekalili huu si muziki, mtaishia hapa hapa tu hamuwezi kuvuka mipaka ya nchi kwa style hii.


    Madirector wa muziki wa taarab hebu jaribuni kubadilika kidogo, ni vyema basi mkawa mnaiga taarab asilia lakini sio kutuletea dansi ndani ya muziki wa taarab, mnakopi alafu mnakaa na kujisifu kwamba ninyi ni  madirector bora! hebu oneni aibu! umizeni vichwa tengenezeni muziki kwa ubunifu wenu na hapo ndipo mtakapoitwa madirector bora, hawa wenzetu wa dansi wamekuwa wakiiga sikatai lakini wao wanaiga kutoka kwenye dansi hiyo hiyo hata kama ikiwa kutoka kongo, lakini hawana cha kuiga kutoka kwenye taarab hii ni aibu!, ujumbe huu leo ni maalum kwa waongozaji wa muziki wa taarab nchini!, tunahitaji mabadiliko tumechoka kusikia dansi ndani ya muziki wa taarab!...Siku zote msema kweli ndio mchukiwa na wengi ila mimi sijali ujumbe umewafikia...Ramadhan kareem!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni