TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 23 Juni 2015

NI VYEMA IKAANZISHWA TUZO ZA TANZANIA TAARAB MUSIC AWARD'S "T.T.M.A." ILI KUPUNGUZA MALALAMIKO YA WADAU!.



NA KAIS MUSSA KAIS
        
MARUDIO:-

           Asalaam aleykum wapenzi wasomaji wangu wa blog hii bora ya www.pambezataarab.blogspot.com kwanza niwatakie mfungo mwema wa Ramadhan kwa wale waislam na wasio waislam nawatakia heri na fanaka pia katika maisha yao ya kila siku!.


        Tumekutana katika makala ya wiki kama ilivyo ada yetu, na kikubwa ambacho nitakizungumzia leo ni kuhusu mchakato mzima n umuhimu wa kuanzishwa kitu kinachoitwa tuzo za Tanzania taarab music award's [T.T.M.A.]. Mashindano haya yakiandaliwa yatapunguza malalamiko toka kwa wadau, wamiliki na wasanii wenyewe husika kwani kumekuwa na malalamiko karibia kila mwaka kutoka kwenye familia hii ya taarab nchini. Yatakapoandaliwa mashindano haya kutakuwa na kategoli nyingi sana na zote zitakuwa zinahusiana na taarab tu, kwa hali hii ina maana hata zile bendi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri na kupendwa na wapenzi na hazionekani kule upande wa pili, huku kwenye "T.T.M.A." zitakuwepo.


   Naamini kutaongezeka kategoli ambazo zitakuwa zikileta hamasa kwa wadau na wasanii, mfano kama vile Director bora wa mwaka, Msanii anae chipukia wa mwaka wa kike mmoja na wakiume mmoja, Bendi bora yenye nidhamu ya mwaka, Mpiga kinanda bora wa mwaka, muimbaji bora wa taarab asili, Tuzo ya heshima kwa waasisi wa muziki huu wa taarab nchini tanzania, na baadhi ya kategoli zingine ambazo kule upande wa pili hakuna, hii italeta hamasa kwa bendi zote na msisimko mkubwa katika tasnia hii ya taarab nchini tanzania.


      Na jambo hili halishindikani kufanyika, nitatolea mfano wenzetu wa bongo movies wanazo tuzo zao kila mwaka "Bongo movies award's", lakini pia wapo katika tuzo zingine ambazo huwa zinachanganywa na wengine wa media mbalimbali ambazo zimepewa jina la "Tuzo za watu" na wala hakuna kinachoharibika, sasa kwanini kwetu sisi watu wa taarab ishindikane?, Endapo kweli zitaanzishwa Tuzo za taarab pekee tanzania hii, basi muziki huu utapata heshima kubwa tanzania na hata nje ya mipaka ya tanzania. nayaomba makampuni na watu binafsi wenye uwezo wa kufanya jambo hili kuanza mchakato mara moja na mafanikio yake watayaona!. Taarab ina wapenzi wengi sana tena wa rika tofauti tofauti!.


   Hebu jaribu kufanya uchunguzi wako japo kijuu juu tu ni redio ngapi ambazo zina vipindi vya taarab hapa nchini tanzania?, na ni makampuni mangapi ambayo yamekuwa yakidhamini vipindi hivyo na kulipa mamilioni ya pesa katika redio hizo kwa muziki wetu huu wa taarab?, hii yote inaonyesha wazi kwamba muziki huu unapendwa sana na watanzania na waafrika kwa ujumla, taarab inazidi kuzagaa afrika na sasa ipo hadi uganda na habari nimeiandika mimi mwenyewe hapa pambezataarab.blogspot.com sasa kipi kitakutisha kuwekeza katika Tuzo za taarab kama hizi endapo tu uwezo unao?, makampuni makubwa na watu binafsi wenye uwezo narudia tena hebu wekezeni katika tuzo hizi za Tanzania taarab music award's [T.T.M.A.] na mafanikio mtayaona, niwatakie Ramadhan kareem na kama utakuwa na lolote basi unaweza kuwasiliana nami kwa namba zangu hizo hapo juu au Email pambezataarab@gmail.com SIKU NJEMA!...MAKALA HII NIMEIRUDIA KUTOKANA NA UMUHIMU WAKE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni