Uongozi wa bendi ya Gusagusa min bendi umelazimika kutoa tamko rasmi la kukanusha kwa mashabiki na wapenzi wake waishio mkoani tanga juu ya habari zilizozagaa humo kwamba bendi hiyo itakuwepo hapo siku ya jumamosi kwa show maalum habari hizo si za kweli!.
GUSAGUSA MIN BENDI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA. |
Wakizungumza na mtandao huu viongozi wakuu wa bendi hiyo Hassan Farouk, Foni Chupa na Kais mussa kais kwa pamoja walisema tumesikitishwa sana na taarifa zilizo zagaa mkoani tanga kwamba tutakwenda kufanya show sisi kama Gusagusa min bendi, hizi taarifa si za kweli kabisa na tunapenda kuwaasa wakazi wa mkoa wa tanga waelewe wazi kuwa hiyo inayokuja huko tanga sio Gusagusa original, ni feki ila wameamua kutumia jina letu kwakuwa wanajua sisi tuna mashabiki wengi huko tanga!.
SABAHA SALUM MUCHACHO AKIIMBA NA GUSAGUSA MIN BENDI. |
Sisi tunapenda kuwaambia wadau wetu kuwa lolote litakalo tokea katika show hiyo hatutohusika nalo na wajihadhari sana na hilo.vile vile tunawaomba hao wanaopenda kutumia jina letu katika shughuli zao waache mara moja kabla sheria haijachukuwa mkondo wake, kumekuwa na tabia hii kwa baadhi ya bendi hapa jijini, kutumia jina la bendi yetu. Uongozi wa gusagusa min bendi tunakemea kabisa tabiaa hii na waache mara moja kuanzia sasa. kitengo cha nidhamu na haki za wasanii pale "BASATA" tayari tumewapelekea malalamiko haya na wameahidi kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo walimalizia kwa kusema viongozi hawa.
KHADIJA KIBAIYA NA ASHURA MLAMALI WAIMBAJI WA GUSAGUSA. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni