TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 20 Juni 2015

VIJUKUU WA TEGO:- TUMEKUJA KUTAMBULISHA "MIN TAARAB STYLE" NDANI YA MAMA WA KAMBO ILI NA WENGINE WAIGE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

       Omary tego, Maua tego na Yusuph tego kwa pamoja ndugu hawa watatu toka coast modern taarab  wamekuja na kitu kizuri ambacho kinaonyesha kitakuwa na mafanikio zaidi hapo mbele ya safari, wameanzisha project ya music kwa vijana wao wawili ambayo wameipa jina la "vijukuu vya tego".

KHAIRAT TEGO NA TALICK TEGO WAKIWAKILISHA VIJUKUU WA TEGO.

    Vijana hawa Talick tego na Khairat tego wamekuja na wimbo wao mpya unaoitwa "mama wa kambo" ambao unatamba kwa sasa katika redio mbalimbali tanzania na nje ya tanzania, ikumbukwe huu ni utunzi wake El-hatibu rajabu, nilipata nafasi ya kufanya mahojiano na vijana hawa ambao wanaonekana wachangamfu na wadadisi wa mambo! nilianza na Talick tego ambae ni mtoto wa Maua tego, yeye alikuwa na haya ya kusema:-


VIJUKUU WA TEGO HAPA WAKIREKODI WIMBO WAO WA MAMA WA KAMBO.

       Mimi naitwa Talick tego nina umri wa miaka12 na ninasoma darasa la nne katika shule ya mtoni primary school, mimi kabla ya Mama na mjomba kunieleza jambo hili la kuimba, mwenyewe nilikuwa naimba mitaani na watoto wenzangu ijapokuwa sikuwa na mawazo kama nitakuja kuimba kama hivi, nilipopewa wimbo huu wa "mama wa kambo" niufanyie mazoezi ilinichukuwa mwezi mmoja ndipo ukanikaa kichwani!, namshukuru mungu tulirekodi vizuri, ila tokea wimbo umetoka na kusikika nimekuwa nikisumbuliwa na watoto wenzangu wakiniambia nimeimba vizuri, nimekuwa nikitazamwa sana kila ninapokuwa naelekea sehemu kama nimetumwa na mama!. Kuna mwalimu anaitwa mwalimu "Kalembo" amekuwa akinipongeza sana na kunipa moyo kila ninapokutana nae!. vile vile pamoja na kuimba lakini pia shuleni kitaaluma nafanya vizuri pia, katika mtihani uliopita nimeshika nafasi ya 4 kati ya watoto 255.


VIJUKUU WA TEGO HAPA WAKIWA NA PRODUCER WAO MAN WALTER NDANI YA STUDIO.

  Nae khairat tego ambae ni mtoto wa Omary tego the special one nilipozungumza nae alikuwa na haya ya kueleza:- kwa jina naitwa khairat tego, nina umri wa miaka 11 nasoma darasa la tano Al-hassan mwinyi primary  school, kwa mara ya kwanza nilipoambiwa na Baba kwamba natakiwa kuimba nilijipa moyo na kumuomba mungu nisimuangushe mzazi wangu sababu alionyesha kuniamini sana, pamoja na hayo lakini pia mimi mwenyewe nilipenda sana kuimba na alienivutia katika uimbaji ni Baba yangu mzazi Omary tego. Wakati tunarekodi ule wimbo niliingiwa na woga baada ya kuvaa yale ma-headphone masikioni lakini baba alinitia moyo na kunipa ujasiri mpaka nikaweza kurekodi vizuri, nashukuru mungu mapokeo ya wimbo wetu kwa jamii ni mzuri sababu kama mimi nimekuwa nikipongezwa sana mitaani na watoto wenzangu na hata watu wazima, malengo yangu ya baadae ni kuwa msanii msomi sababu napenda sana shule pamoja na kuwa naimba, napenda niwe kioo cha jamii na niweze kuwasaidia wajane na yatima ila kubwa zaidi nataka kuwa msanii wa kimataifa zaidi.


  Meneja wetu Yusuph tego au kama tunavyomuita "Uncle meneja" amekuwa akitufundisha taratibu za kuimba, muimbaji anatakiwa awe vipi, kitu gani muimbaji hatakiwi kutumia, pia ametuletea mwalimu ambae anatufundisha kucheza mitindo mbalimbali ya muziki anaitwa mwalimu "Kijibwa".


MENEJA WA VIJUKUU WA TEGO, YUSUPH TEGO.

  Nae meneja wao Yusuph tego alisema kuwa tumeamua kuleta kitu tofauti kidogo kwa jamii hususani wapenda taarab, sisi tumekuja na mtindo mpya ambao tumeupa jina "Min taarab style" hapa tunatengeneza wimbo wenye dakika sita tu lakini wenye mahadhi ya taarab, hata ukiusikia wimbo wao utakuta una dakika sita tu na sekunde kadhaa!, watoto hawa tumewatengea muda wa kusoma na kufanya mazoezi ya kuimba, muziki ni week-end tu!, siku zingine zote ni masomo kwa kwenda mbele. jumatano ijayo tunatarajia kufanya shooting ya wimbo huu na mdhamini mkubwa wa shooting hii ni "Nassoro Chege" ambae yupo kule nchini uingereza maeneo ya Manchester huyu jamaa tunamshukuru sana kwani amekuwa mstari wa mbele sana katika kututia moyo, kutusaidia na hata kutupa ushauri pia mungu ambariki sana.

MKURUGENZI WA VIJUKUU WA TEGO, OMARY TEGO "THE SPECIAL ONE!".

  Mkurugenzi Omary tego akimalizia alisema kuwa anawashukuru wadau wote kwa mapokezi yao mazuri kwa vijana wao kuanzia watangazaji wa redio, Wandishi wa mitandao mbalimbali kama ubuyuwataarabutz.blogspot.com wandishi wa magazeti mbalimbali watu wa Tv ambao kila kukicha wamekuwa wakitaka video ya wimbo huu wa mama wa kambo na wengineo wote sitoweza kuwataja majina wote ila tunashukuru sana. wajiandae na shooting yetu pamoja na wimbo mwingine mpya toka kwa vijana hawa!.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni