TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 1 Julai 2015

BONGO STAR'S MODERN TAARAB, HATUIMBI NYIMBO KWA AJILI YA TEMBA, TUPO KUELIMISHA JAMII!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

         Bongo star's modern taarab ni bendi mpya iliyozaliwa baada ya iliyokuwa Fungakazi modern taarab kumeguka vipande viwili na kuzaliwa bendi hii mpya!, mkurugenzi wa bendi ya Bongo star's modern taarab anaitwa Senior Bachelor na wa fungakazi modern taarab anaitwa kapteni temba mchaga wa kwanza kuimba taarab!.

SENIOR BACHELOR MKURUGENZI WA BONGO STAR'S MODERN TAARAB.

      Mpaka sasa bendi hii wameshatoa vibao vyao viwili ambavyo ni Fisadi kafilisika ulioimbwa nae Salama sambwanda na tayari nimeuweka katika hii blog, na ya pili Funga domo ambayo imeimbwa nae Salma mikausho!, mtandao huu ulipata habari kwamba bendi hii imekuwa ikitunga nyimbo zake kwa ajili ya kumlenga mkurugenzi wa fungakazi modern taarab kapteni temba, ndipo tulipoamua kumtafuta mtunzi na mkurugenzi wa bendi hii ya Bongo star's modern taarab Senior Bachelor aelezee je kwanini amekuwa akifanya hivyo?.


      Nilimtafuta kwa njia ya simu na haya ndio maelezo yake ambayo alinijibu, Unajua ndugu yangu kwakuwa mimi nilikuwa fungakazi na Temba kipindi kile na kwa sasa nimehama nipo na bendi yangu basi hata nikiandika shairi la aina gani wapenzi na wadau wanasema nimeamua kumuimba temba, lakini mimi kama mtunzi wa nyimbo hizo na mkurugenzi wa bendi hii nasema sikutunga nyimbo hizo kumlenga temba hapana! yeye ana maisha yake na mimi pia nina maisha yangu hii bendi ipo kwa ajili ya wanajamii wote natunga nyimbo kuelimisha jamii inayotuzunguka


SALAMA SAMBWANDA MUIMBAJI WA BENDI YA BONGO STAR'S MODERN TAARAB.

   Napenda niwaambie wapenzi wote wa taarab kuwa mimi nimeondoka Fungakazi wala sio kwa ugomvi na hata temba nilimuaga na akaridhia nipo katika kutafuta maisha yangu mimi mwenyewe naomba nieleweke hivyo kwa yeyote ambae atahitaji huduma za bendi hii basi anaweza kunipigia simu yangu ya mkononi ambayo ni 0719-626 805 alimaliza kwa kusema!.


     Ukizisikiliza nyimbo hizi mbili za Bongo star's modern taarab mashairi yake yalipolalia ni lazima uamini kuwa alielengwa hapa ni Temba, hata huu mwingine wa Funga Domo ulioimbwa nae Salma Mikausho nao una maneno ambayo yanasemekana ni madongo kwa temba, nawaahidi wasomaji wangu jiandaeni kuusikiza na huu wimbo wa pili "Funga Domo" nitauleta hapa hapa nanyi mupate kuusikia na kutoa maoni yenu unauonaje?. Huu ndio mtandao bora wa taarab kwa sasa huwa haufichi kitu....Tusubiri!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni