TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 25 Julai 2015

DIAMOND PLATINUM KUURUDIA WIMBO WA "ASSU" SAMBAMBA NA ABDUL MISAMBANO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Diamond platinum amevutiwa na wimbo wa Assu na kupanga kuurudia tena kisasa zaidi  akishirikiana na muimbaji husika Abdul misambano mwenyewe, wimbo huu ulirekodiwa na bendi ya Babloom na ukaimbwa na misambano hapo miaka ya nyuma.


DIAMOND PLATINUM.

          Misambano alisema kuwa nilipokea simu ya Diamond platinum akiniomba kuurudia tena wimbo wangu na alichokisema ni kwamba anataka tuuimbe sote kwa pamoja yaani mimi pamoja na yeye, kwahiyo nasubiri Diamond atakapokuwa tayari basi muda si mrefu kutoka sasa tutaufanya wimbo huu na wapenzi watapa radha tamu toka kwetu kwa pamoja!.


       Diamond amekuwa ni msanii ambae amekuwa akibadilika kwa kufanya aina mbalimbali za muziki na hii yote ni katika kudhihirisha kwamba yeye ni muimbaji na msanii waukweli ambae ana uwezo wa kufanya muziki wa aina yoyote ule, wadau tusubiri kusikia wimbo huo nini atafanya sababu amekuwa si mtu wa kubahatisha katika nyimbo zake zote!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni