Wimbo uliokuwa gumzo kwa muda mrefu midomoni mwa wapenzi na wadau wa taarab afrika mashariki na kati "Najuta kupenda" ulioimbwa nae "Asya mariam" akiwa na wakaliwao modern taradance unarajiwa kutambulishwa katika vyombo vya habari kesho jumapili tarehe 26/7/2015.
Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa wakaliwao modern taradance Thabit Abdul mkombozi alisema niliahidi kutoa wimbo huu mpya baada ya mwezi mtukufu wa ramadhan kuisha na sasa natimiza ahadi yangu kwa wapenzi na wadau wa taarab nchini tanzania na duniani kwa ujumla. Ikumbukwe kuwa huu ni muendelezo wa ule wimbo wa Asya utamu wa "Siioni thamani ya pendo" unaotamba katika vyombo vya habari kwa sasa!.
ASYA MARIAM "UTAMU" MUIMBAJI WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE!. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni