TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 25 Julai 2015

GUSAGUSA MIN BENDI KUSHUSHA BURUDANI YA NGUVU LANGO LA JIJI MAGOMENI MIKUMI JUMAMOSI YA LEO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                 Bendi yako uipendayo ya Gusagusa min bendi wazee wa uingereza "full handas...full nakhwa" leo siku ya jumamosi wanatarajia kushusha burudani ya nguvu katika ukumbi wao wa nyumbani wa lango la jiji magomeni mikumi jijini Dar.


WAIMBAJI WA GUSAGUSA MIN BENDI, WAKIONGOZWA NA BI AFUA.

          Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo mr Hassan Farouk amesema kwamba baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kupisha mwezi mtukufu wa ramadhan na ile funga ya sita, leo wanarudi tena kuwapa burudani muruwa wapenzi wake ambayo walikuwa wamei-imiss kwa takribani mwezi mmoja na siku kadhaa.


      Ninawaomba mashabiki na wapenzi wetu kujitokeza kwa wingi ili kuja kupata burudani nzuri toka kwetu alimalizia, Gusagusa ni bendi inayopiga nyimbo za zamani za taarab yaani zile "Old is Gold" pamoja na nyimbo zao wenyewe ambazo wamezirekodi, ni bendi iliyo na wapenzi wengi sana kwa sasa hapa jijini Dar na vitongoji vyake!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni