TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 23 Julai 2015

TETESI:- SHABBAN KINANDA AREJEA COAST MODERN TAARAB KINYEMELA NA KUITOSA OGOPA KOPA CLASSIC KISA...........!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Mpiga kinanda anaechipukia kwa kasi Shabban kinanda, inasemekana amerejea katika bendi yake ya zamani Coast modern taarab kinyemela akitokea Ogopa kopa classic ambayo amejiunga nayo miezi minne iliyopita.


SHABBAN KINANDA AKIWAJIBIKA!.

        Taarifa zinaendelea kusema kuwa mpiga kinanda huyo alianza kuwadengulia ogopa kopa classic bendi tokea siku ya sikukuu ya Idd mosi ambapo hakutokea kabisa ogopa kopa walipokuwa wakifanya show yao kimanzichana, siku ya Idd pili wakati ogopa kopa wanapiga ikwiriri mkoani pwani inasemekana Shabban kinanda alionekana kibiti ambapo kulikuwa na show ya Coast modern taarab.


    Siku ya jana ambapo ogopa kopa walikuwa wakisafiri kuelekea arusha na mombasa pia Shabban kinanda hakuonekana wala kutokea eneo la safari. na tetesi za chinichini zilizozagaa kwa wanamuziki kadhaa zinasema kuwa Shabban kinanda amekwama kimapenzi kwa muimbaji mmoja ambae yupo pale Coast modern taarab ambae inasemekana anatoka nae, hali inayompelekea kutokuwa na msimamo katika kazi yake!.


    Tulipomtafuta Shabban kinanda ili kuzungumzia hili hakupatikana katika simu yake ila tunawaahidi wasomaji wetu kwamba tutamtafuta Shabban kinanda ili aweze kulizungumzia hili na kuliweka bayana wadau na wapenzi mmlijue.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni