Bendi yako uipendayo ya jahazi modern taarab inatarajia kufanya uzinduzi wa albam yake ya "mahaba niue" mwezi wa nane mwaka huu ila tarehe rasmi na wapi itakuwa bado imeendelea kuwa siri kidogo!.
Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo Mzee yusuph alisema, ndani ya albam hiyo kutakuwa na nyimbo sita na itakayobeba albam ndio hiyo mahaba niue! alizitaja nyimbo hizo kuwa ni:-
FATMA SHOBO AKIWAJIBIKA STEJI. |
1.Hili tu limekuuma, utakaoimbwa na Fatuma shobo
2.Kamwe sitoumbuka, utakaoimbwa na Fatuma kassim
3.Nina moyo sio jiwe, umeimbwa nae Leyla rashid "malkia".
4.Nia safi hairogwi, utakaoimbwa nae Mishi mohamedy
5.Mahaba niue, ulioimbwa nae Mzee yusuph "mfalme".
6.Ni wimbo utakaoimbwa na muimbaji wa kiume kati ya Twaha malovee, Prince amigo au Mtoto pori mmoja yao atapewa wimbo ili kujaza albam na kufanya nyimbo kutimia sita!.
KHADIJA YUSUPH "SAUTI YA CHIRIKU" AKIFANYA YAKE!. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni