TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 30 Julai 2015

MPIGA KINANDA WA GUSAGUSA MIN BENDI AFIWA NA BABA YAKE MZAZI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

               Mpiga kinanda wa kutegemewa wa bendi gusagusa min bendi ya jijini dar Hamisi chizi almaarufu amefiwa na baba yake mzazi huko visiwani zanzibar.


MPIGA KINANDA WA GUSAGUSA HAMISI CHIZI AMBAE AMEFIWA NA MZAZI WAKE.

           Mzee amefariki jana saa kumi na mbili jioni na panapo majaaliwa tunatajia kumzika leo saa saba mchana huko muungoni shambani kwetu visiwani unguja. mzee alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda sasa, kikubwa nawaomba ndugu jamaa na marafiki tushirikiane kwa pamoja ili tuweze kumfikisha mzazi wangu katika safari yake ya mwisho, kwani naamini safari hii ni yetu sote binadamu.


        Uongozi wa bendi ya gusagusa umesafiri visiwani humo tayari kwa kushiriki na msanii huyo kwenye mazishi ya mzazi wake yatakayofanyika siku ya leo. Mkurugenzi wa mtandao huu kais mussa kais na watendaji wote kwa ujumla wanatoa mkono wa pole kwa msanii huyo kwa kufiwa na mzazi wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni