TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 31 Julai 2015

PAMOJA NA KUHAMA KWA SALHA WA HAMMER 5 STAR'S MODERN TAARAB, VIDEO YA WIMBO KISHTOBE KWENDA HEWANI TV ZOTE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Siku chache zilizopita msanii salha wa hammer alitangazwa na uongozi wa wakaliwao modern taradance kuwa tayari amejiunga na bendi hiyo na kuipa kisogo bendi yake ya zamani ya 5 star's modern taarab.


ALLY J MKURUGENZI WA 5 STAR'S MODERN TAARAB.

      Dawati la habari la mtandao huu makini uliamua kumtafuta mkurugenzi wa 5 star's modern taarab Ally J nia ni kutaka kujua vipi kuhusu video mpya ya wimbo kishtobe ulioimbwa na salha na bado haujapelekwa katika televisheni mpaka sasa je utapelekwa au mkurugenzi atafanya nini? kwanza kabisa napenda nikueleze kuwa video ya wimbo ule itapelekwa katika televisheni mbalimbali bila kujali kuwa salha ameihama 5 star's ama lah! alisema.


       Huu wimbo ni wa bendi ya 5 star's modern taarab na wala sio wa salha hivyo naweza kufanya chochote kile, hata kama huko alipokwenda atapewa wimbo mwingine lakini huu nitaupeleka katika televisheni zote kama nilivyopanga awali, mimi huwa sina utaratibu wa kufuta wimbo pindi msanii anapokuwa amehama bendi, haya ni maisha tu, mtu ana uhuru wa kuamua atakacho alimaliza kwa kusema.


   Ikumbukwe kuwa muimbaji salha wa hammer ameihama bendi ya 5 star's modern taarab na kujiunga na wakaliwao huku akiwa na video mpya kabisa ambayo ilikuwa bado haijatoka kabisa na kutambulishwa katika televisheni mbalimbali.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni