NA KAIS MUSSA KAIS.
Uzinduzi wa albam ya pili toka bendi ya wakaliwao modern taradance "sioni thamani ya pendo" ulifana na kufunika zinduzi zote zilizowahi kufanyika kipindi cha hivi karibuni, umati mkubwa uliojitokeza uliwashangaza wengi na kutabiri kuwa bendi hii italeta ushindani wa kweli kwa bendi kongwe za taarab nchini.
Show ilianza saa mbili kamili kwa bendi ya exellent modern taarab chini yake mwinyi mkuu na maina thadei kupanda steji na kupiga nyimbo sita mfululizo zilizowapagawisha mashabiki lukuki waliojitokeza, ilipofika saa nne na nusu walipanda ogopa kopa classic bendi chini yake malkia khadija omary kopa ambao nao walipiga nyimbo zaidi ya nne nakushangiliwa sana.
Saa tano na nusu alipanda msagasumu ukipenda muite mkali wa radha ambae aliwapagawisha na kuwarusha haswa watoto wauswahilini na nyimbo kama rafiki wa kweli na nyinginezo nyingi. saa tano na dakika arobaini na tano alipanda Juma nature au ukipenda muite mfalme wa temeke ambae alitumbuiza mpaka saa sita na nusu walipopanda jahazi modern taarab, nao waliwadatisha mashabiki kwa nyimbo zao takribani sita mfululizo na ilipofika saa nane ndipo uzinduzi rasmi ukafanyika kwa mkurugenzi wa bendi ya wakaliwao kubebwa juu juu katika kiti cha kifalme na kupelekwa moja kwa moja mpaka stejini huku sebene kali sana likitumbuizwa na wanamuziki wa bendi hiyo
Alipofika stejini thabit abdul alicheza sebene sambamba na wacheza viduku huku mkurugenzi huyo akionekana kwenda sambamba kiuchezaji na vijana wake, baada ya kama dakika sita kupita tokea thabit abdul kufika stejini ilisikika ngoma ya mdundiko ikirindima tokea upande wa geti la kuingilia dar live jambo lililowafanya mashabiki kunyanyua vichwa vyao ili kuangalia kulikoni?, ndipo alipoonekana Asya mariam akiwa amebebwa mabegani huku akinema kama mwali wa kizaramo, mdundiko huo ulisogea huku mwali akinema mpaka stejini na baada ya kufikishwa hapo Asya mariam ikapigwa ngoma ya vanga na kuwafanya mashabiki kupagawa na kuanza kucheza sambamba na mwali huyo Asya mariam!.
|
|
Asya mariam aliimba wimbo wake wa sioni thamani ya pendo huku akiwa katika mavazi yale yale ya mwali wa kizaramo na kulia sanaa!, baadhi ya wapenzi nao walianza kulia na kusema wimbo huo unawaliza sababu umejaa maneno ya kweli na yanayotokea kwenye jamii. wakaliwao walipiga nyimbo tatu na kumpisha dogo jack simela muimbaji wa muziki wa mnanda au mchiriku, aliimba kwa dakika therathini kabla ya wakaliwao kupanda tena na kumalizia, show ilipendeza sana na iliisha saa kumi na nusu alfajiri.
Mtandao huu unapenda kuwapongeza bendi ya wakaliwao modern taradance kwa kikubwa walichokifanya kwani uzinduzi wao ulikuwa bab-kubwa na umewafanya wapinzani wao kuanza kuwahofia na kuwaogopa, jambo la umuhimu kwao ni kukomaa na kuendelea mbele zaidi ili kufikia mafanikio waliojiwekea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni